Ijumaa Wikienda linakupa orodha ya wabunge hao warembo ambapo
waliojulikana kwa kukimbiza kama akina Halima Mdee wametakiwa kukaa
chonjo. Hata hivyo, wabunge warembo wa kike ni wengi, lakini wafuatao
ndiyo ‘shida’ kuanzia maumbo na sura zao.
magige

Rekodi ya urembo wake haijawahi kuvunjwa bungeni. Mara zote, tangu
alipotinga bungeni mwaka 2010, amekuwa gumzo kubwa kwa uzuri wake, licha
ya kushindanishwa na wabunge kadhaa, lakini bado ‘anatusua’ vilivyo.

BONNAH KALUWA (CCM)
Hii ni mara yake ya kwanza kuingia bungeni. Uzuri na urembo wake
umeonekana gumzo bungeni tangu mwanzo hadi mwisho wa kikao hicho. Sura,
umbo na macho yake vimekuwa kivutio kikubwa.
kairuki

ANGELLA KAIRUKI (CCM)
Ukimwangalia vibaya, unaweza kusema ni shombeshombe. Urembo wa sura
yake, umekuwa ukiwapa nyakati ngumu watu wengi, wakati mwingine
kushindwa hata kung’amua kama ana asili ya Kiarabu au la!
Kinachomuongezea sifa katika kilinge cha urembo ni umbo lake
lililojengeka.

ESTER MATIKO (CHADEMA)
Achana na ukali wa hoja zake anapochangia mijadala. Hiki ni ‘kisu’
kikali kinachovutia bungeni. Umbo lake la ‘kitoto’, uzuri wa sura na
macho ya mviringo, vinamfanya aonekane mrembo na mwenye uzuri wa
kupindukia.
bukwimba

LOLESIA BUKWIMBA (CCM)
Tabasamu lake ndiyo limekuwa gumzo. Sura yenye uchangamfu imekuwa
ikiteka macho ya watu wengi. Kamwe huwezi kuchoka kumtazama mwakilishi
huyo. Mpole kama alivyo, lakini amekuwa ‘akikimbiza’ vilivyo mjengoni.
DK MARRY MWANJELWA (CCM)
Licha ya umri kuanza kumpigia honi lakini anawafunika wabunge wengi
wenye umri mdogo. Urefu na figa nzuri, vinachangia kwa kiasi kikubwa
kumweka kwenye orodha ya wabunge wa kike wanaotikisa kwa uzuri.

UMMY MWALIMU (CCM)
Hana makuu. Mpole na mwenye aibu wakati wote, lakini urembo wake
unashereheshwa na umbo lake matata. Ana urembo wa haja unaoyapa macho
kazi ya ziada kuitafuta kasoro yake.

CECILIA PARESSO (CHADEMA)
Urembo, uzuri wa umbo lake, urefu, unene wa wastani na sura nzuri vinatosha kumuingiza kwenye orodha hii.
JULIANA SHONZA (CCM)
Umbo lake ni la kawaida, lakini shughuli iko usoni. Achana na sehemu zingine za mwili, ukimtazama usoni tu utagundua ni kisu.
LUCY MAYENGA (CCM)
Ni mrembo wa umbo na sura. Hahitaji maneno mengi kumwelezea, lakini
ukweli unabaki palepale kuwa ni miongoni mwa wabunge warembo walioupa
shida Mji wa Dodoma.
Mboni-Mhita

MBONI MHITA (CCM)
Akiwa umbali kidogo kutoka mahali ulipo, unaweza kumchukulia kawaida!
Shughuli ipo akikusogelea. Umbo na uzuri wake ni habari nyingine.

NEEMA MGAYA (CCM)
Rangi yake ya asili, ngozi laini, umbo namba nane na ucheshi wake,
vinamtetea kuingia kwenye ulingo wa wabunge hawa warembo zaidi.
VICKY KAMATA (CCM)
Silaha kubwa aliyonayo ni midomo na macho! Geuza gazeti nyuma, mtazame
tena Vicky, unaona? Si umbo, si sura, si macho, si mdomo, Vicky Kamata
ni mrembo. Inatosha kusema hivyo tu.

JESCA KISHOA (CHADEMA)
Ni mrembo anayevutia kwenye viunga vya bungeni na inawezekana ndiyo
maana aliyekuwa Mbunge wa NCCR-Mageuzi, David Kafulila aliamua kuchukua
jumla na kumweka ndani.
bulaya

ESTER BULAYA (CHADEMA)
0 comments:
Post a Comment