,./.,

,,

... ...

';';';';

''=

==

adv
Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Wednesday, November 11, 2015


MAPENZI, UDINI, UDUGU, UKABILA VILITAWALA MCHAKATO WA VITI MAALUM CHADEMA.
 
Mchakato wa viti maalum CHADEMA kuna mawili utakiimarisha chama zaidi au chama kuyumba sana na pengine kufa kabisa.

Nikiwa kama mwanachama na mpenzi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA naumia sana ninapokiona chama changu kipo katika hali ngumu sana, hali iliyosababishwa na mchakato wa viti maalum, nakishauri chama changu No way out kiombe radhi tu kwa wanachama wake ili kukinusuru chama katika hali hii tete, na kisiishie kuomba radhi, lakini pia kiachane na utaratibu huu usio shirikishi katika kupata viti maalum.
Kosa kubwa chama lililofanya mchakato huu haukuwa shirikishi kwa viongozi wa ngazi za chini kikundi cha watu wachache kilijiamulia maamuzi wanayowajua wao bila kusoma mazingira na mtu gani anawakilisha mkoa gani, na je atakuwa ni chaguo sahihi???

Walifanya kwa mazoea sana huku wakiwa wamejisahau chama kimekuwa kikubwa. mamlaka yapo kwa wanachama wenyewe siyo watu wachache waliozoea kujipa umungu mtu ndani ya CHADEMA.

Haka kakundi kimejisahau kabisa kama chama kilitoka ktk wakati mgumu wakupambana na UDINI, UKABILA na UKANDA leo mchakato wa viti maalum katika chama changu umegubikwa na hizi hali ikiwemo kashfa ya ngono na rushwa pamoja na UBINAFSI uliofanywa na Baraza la wanawake BAWACHA TAIFA,

Viongozi wote wa BAWACHA Taifa ni wabunge wa BUNGE lijalo 2015 Kasoro makamu nwenyekiti wa BAWACHA Taifa Zanzibar Bi Halima Juma.

Tunakipeleka wapi Chama Chetu kila mtu analalamika. Viongozi Wa mikoa wanalalamika, viongozi wa Majimbo wanalalamika, viongozi wa Wilaya wanalalamika, viongozi wa Kata wanalalamika na wanachama wa kawaida wanalalamika. Every Body Blame, Why? Mbona vyama vingine havilalamikiwi kwa kiasi hiki.
Kuna Mambo Chama hakijawatendea haki na usawa wanachama wake na ndiyo maana wanalalamika.
Wanaume wanalalamika.
Wanachama wa kawaida wanalalamika.

Ndiyo maana nikasema chama kipo katika hali ngumu sana uwezekano wa kufa ni mkubwa juliko kubaki salama.
Mfano Hivi wanawake wale waliokuwa Tayari kujitoa kwa hali na mali watakuwa na utayari na ari kama zamani kufanya kazi kwa moyo na BAWACHA kama walivokuwa wanafanya kazi hapo awali. BAWACHA Watakuwa ni wageni wa nani huko majimboni kwenye wanachama kufanya nao kazi!!
Hivi Waliwachagua kwaajili ya kuwapa tiketi za kwenda Bungeni ? 
Kwanini Halmashauri kuu BAWACHA Taifa Haikuitishwa na hiyo halmashauri yenyewe ikapendekeza majina ya wabunge wao?
Ubabe wa Halima Mdee kukataa kuitisha Halmashauri Kuu BAWACHA Taifa ili atimize ndoto yake kwa urahisi ya kwenda na baraza lake lote Bungeni pamoja na Mashosti zake unakigharimu sana Chama leo.

Mkoa kama wa Pwani wenye watu wengi wa Imani ya kiislamu , Hivi kweli Watakiona hiki chama na wao ni cha kwao? mpaka mbunge wa mkoa huu akawakilishe Anna Deo Muro (Mchaga Mkristo)

Mkoa Wa Morogoro hivi kweli wale wadada waliokipagania Chama hiki kwajasho lao lote mpaka Wakawakilishwe na Devotha Minja (Mchaga)

Mkoa wa Tanga ni sahihi kuwakilishwa na Yosepher Komba (Mngoni) tena mgeni katika Chama huku wenyeji wenye Tanga Yao na Wapiganaji kama kina Aminatha Saguti Wakiendelea Kuambiwa jengeni chama. Fursa Hawastahili kuzipata katika Mkoa Wao!!

Mkoa kama wa PEMBA juzi tu umetupa kura za heshima kwa mgombea URAISI. Mkoa wa PEMBA Walipiga Kura za Kutosha Kwa Mgombea URAISI wa CHADEMA Mh Lowassa akimuacha mbali Mgombea wa CCM John Pombe Magufuli. Kwa kitendo cha kamati ndogo kumteua Zainab Bakary haikuwatendea haki kabisa wakazi wa Pemba, Hivi kweli watajisikia na wao chama ni cha Kwao??

Zainab ni mtoto wa dada yake Said Mohammed Issa (Makamu Mwenyekiti CHADEMA Taifa Zanzibar) Dada yake tumbo moja kuzaliwa,, hivyo Zainab anamuita Said Issa ami (Mjomba) ,
Zainab numewe ni Naibu Katibu Mkuu BAVICHA Taifa.. Zainab ami yake mwingine ni Khamis Mohammed Issa ambaye ni kaka mkubwa kuzaliwa katika Familia hii na yeye ni Mratibu wa Kanda ya Pwani kila mwezi analipwa posho na CHADEMA na Said Issa naye kila mwezi analipwa posho na CHADEMA,
Hivi wale ndugu zangu wakipemba CHADEMA watakiona na wao ni cha Kwao au ni Saccos Ya Said Issa Kwa Maslahi yake binafsi na familia yake? Mbunge aliyepita viti maalum Mkoa Wa Pemba 2010 Mh Raya alikuwa mtoto wakaka yake na Said Issa, 2015 amemleta mtoto wa dada yake. Kweli CHADEMA hatukua serious kabisa ktk Hili?

Aliyesababisha Tukose Jimbo Segerea Anatropia anazawadiwa UBUNGE viti naalum kwasababu tu anamahusiano ya kimapenzi na mkurugenzi wa BUNGE na Halmashauri John Mrema. Kwa ujumla wale ambao walikuwa na mahusiano ya karibu na viongozi wa makao(sio ya kikazi) ndio wamependelewa viti maalum.
Ni lazma tujiulize wanachadema Wenzangu . Jambo Dogo tuu la mgawanyo wa viti maalum uliozingatia haki na usawa limetushinda, Ndiyo kwanza viongozi wetu wametanguliza UDINI, UKANDA, UKABILA na MAPENZI.

Je wananchi wangetuamini kutupa nchi ingekuwaje? Lazma tujipime na tujitafakari kwa kina.
Niishie hapa kwa leo Illa ukweli utabaki palepale chama chetu CHADEMA kinaelekea kufa au kuimarika zaidi kama mapungufu haya yakifanyiwa kazi!

Hata hivyo, tukisamehe chama chetu na tuzidishe maombi , kama ni mgonjwa yuko mahututi.
 
bY mrishorahma4@gmail.com

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi