
Chama cha mpira wa miguu mkoa wa Temeke TEFA kimefanya uchaguzi wa viongozi wake kimyakimya licha ya kuwepo na amri ya mahakama kusitisha uchaguzi huo usiendelee kutokana na mmoja wa wagombea wa nafasi katika uchaguzi huo kufungua mashtaka dhidi ya viongozi wanaosimamia uchaguzi huo.
TEFA kupitia kwa afisa habari wake Benny Mwanantara jana usiku walitoa taarifa rasmi ya kufanyika kwa uchaguzi huo na kuwataja baadhi ya viongozi ambao walichaguliwa kwenye uchaguzi huo licha ya mwenyekiti wa DRFA Almasi Kasongo kuthibitisha kupokea agizo la mahakama ya Temeke kwamba uchaguzi huo umesitishwa hadi mahakama hio itakapotoa maamuzi juu ya shauri lililofunguliwa mhakamani hapo.
Tarifa kutoka kwa Mwanantara ambaye ni Afisa habari wa TEFA inasomeka kama ifuatavyo;
“Uchaguzi wa TEFA wafanyika, wanachama 76 wamrudisha kwa kishindo mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Temeke (TEFA) Peter Mhinzi makamu wake ni Mohamed Salehe na wajumbe ni Fikiri Magoso, Ally Kulita na Sele Kikambi”.
Mwanatara amesema uchaguzi huo ulifanyika kwa amani maeneo ya Chamazi-Mbagala, Dar es Salaam na viongozi wa chama cha soka mkoa wa Temeke wamepatikana.
Kabla ya taarifa hiyo kutoka, kituo cha Clouds FM kilifanya mahojiano na mgombea nafasi ya ujumbe wa TEFA Fikiri Mgoso akasema alikuwepo sehemu ambapo awali ilipangwa kufanyika uchaguzi huo ambapo ni Navy Beach Kigamboni lakini alilazimika kurudi nyumbani baada ya kukuta eneo hilo likiwa halina watu kwa ajili ya shughuli za uchaguzi.
Kwahiyo kama uchaguzi wa TEFA ulifanyika inamaanisha Fikiri Magoso amechaguliwa bila yeye kuwepo kwenye uchaguzi huo.
Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Dar es Salaam Almasi Kasongo siku ya Ijumaa alitangaza kupokea ya mahakama kusitisha uchaguzi wa chama cha soka mkoa wa Temeke TEFA. Mahakama ya Temeke ilizua uchagui huo baada ya kufunguliwa kwa shauri dhidi ya mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya TEFA, mweniki wa kamati ya uchaguzi ya DRFA na mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya TFF.
Lakini pia mwenyekiti wa uchaguzi wa TEFA Bw. Rashid Salada alikiri kupokea taarifa kutoka mahakama ya Temeke inayozuia uchaguzi huo usifanyike siku ya November 22, 2015 kutokana na kuwepo kwa shauri mahakamani linalohusu uchaguzi huo.
0 comments:
Post a Comment