Yamekuwa
hayo? Aliyewahi kuwa mwandani wa staa wa Bongo Fleva Nasibu Abdul
‘Diamond Platnumz’, Penniel Mwingilwa `DVJ Penny’ amegoma kuulizwa
chochote kuhusu kitendo cha zilipendwa wake huyo kupata mtoto wakati
yeye alidaiwa kukataa kumzalia.
Akizungumza
na Ijumaa Wikienda, wikiendi iliyopita, Penny alifunguka kwamba, haoni
kama kuna sababu ya kumzungumzia Diamond na mtoto wake (Tiffah) kwani
walishaachana zaidi ya miaka miwili sasa.
“Jamani, huyo mtu kwa sasa hanihusu na sioni kama kuna sababu ya kumuongelea mtoto wake, anayepaswa kuulizwa mambo ya Diamond ni Zari, kwa hilo mnisamehe (no comments), nikiulizwa niulizwe mambo yangu tu,” alisema Penny.
GPL

0 comments:
Post a Comment