,./.,

,,

... ...

';';';';

''=

==

adv
Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Wednesday, June 24, 2015


BAADA ya mizunguko ya wiki nzima, ni Jumamosi nyingine tulivu tunakutana waungwana kuweza kupata darasa huru la uhusiano.
Kwa wale tuliokuwa pamoja wiki iliyopita tuliweza kujifunza kuhusiana na jinsi ya kuishi katika ulimwengu huu ambao kila mtu amejeruhiwa na mapenzi.
Hakika uliweza kung’amua unapaswa kuishi vipi ili uweze kupata mwenza sahihi na usiendelee kujeruhiwa kila uchwao. Nawashukuru sana wote mlioguswa na mada ile na kuweza kunitumia ujumbe mfupi. Tuendelee kuwa pamoja.


Leo nakukaribisha nikiwa na mada mpya mezani. Kama inavyojieleza hapo ni ukweli usiopingika kwamba unapompenda mtu huwa unakuwa hauko tayari kumpoteza. Utafanya kila linalowezekana kuhakikisha anaendelea kuwa wako, huo ndiyo upendo wa kweli.

Wengi wetu tumeshakutana na hali hii. Hali ya kumpenda mtu hadi kupitiliza. Unapenda kumuona mpenzi wako ana furaha na amani muda wote. Unaishi naye kwa muda wa mwaka mmoja lakini unamzoea utadhani mmeishi naye kwa miaka kumi na mitano.

Hapo unasahau kabisa kwamba lolote linaweza kutokea wakati wowote. Akili yako haiwazi hata siku moja kwamba mwenzako anaweza kuvutiwa na mtu mwingine na akakuacha solemba.

Kamwe hufikirii kwamba mpenzi wako anaweza kuwa anakuongopea na kujifanya anakupenda kumbe akili yake haipo kwako. Ulimwengu wa sasa umebadilika. Inahitaji akili ya ziada kumjua mtu mwenye mapenzi ya dhati.

Mtu anaweza kukuoneshea machoni kuwa anakupenda kumbe moyoni ana lake jambo. Anaye ampendaye. Wewe anakuzuga tu. Anaweza kukuzuga kwa sababu ana masilahi fulani katika penzi lako.

Yawezekana anapata fedha, yawezekana anataka sifa kwamba ana mpenzi mzuri mbele ya jamii na mambo mengine mengi yanayofanana na hayo.

Mtu wa aina hiyo huwa hawezi kuguswa hata kidogo na maumivu yako.

Anachoangalia yeye ni nini anakitaka kutoka kwako. Atakapoona amekipata, ni rahisi tu kukwambia nenda zako. Ni rahisi sana kukwambia hakuhitaji.

Hana cha kupoteza, ameshakunyonya na kukudanganya vya kutosha. Kutokana na mazoea uliyojijengea, si rahisi kukubaliana na kauli ya kwamba hakutaki.

Nguvu ya upendo ndiyo itakayokuendesha. Unakuwa hujielewi wakati huo, unapambana kwelikweli kuhakikisha anaendelea kuwa wako. Utatafuta hadi umpate anayetibua penzi lako.

Bahati mbaya kumjua kwako pia hakusaidii kitu. Inafika wakati anakuambia umuache aendelee kufurahia penzi lake. Bado tu unakuwa huelewi kitu. Unageuka mtumwa na si mpenzi au baby mlivyokuwa mkiitana zamani.

Unafikia wakati eti unamsaka mtu ambaye yupo na mpenzi wako ili umuoneshe. Umueleze kwamba amekuibia. Bado inakuwa haisaidii,

anakudhalilisha tu. Anakuambia hana mpango na wewe, unaendelea kuteseka. Unajifungia ndani unalia usiku kucha. Unamlilia mtu ambaye hathamini hata chembe ya chozi lako.

Huo ni utumwa. Ikifikia hatua hiyo ni vyema ukaanza kukaa mbali na mtu huyo. Hujazaliwa naye. Mmekutana tu ukubwani. Utamsahau. Watu wanasahau maumivu ya kuwapoteza ndugu zao waliotangulia mbele za haki sembuse huyo mliyekutana ukubwani?

Jiweke naye mbali kwa kufanya mambo ambayo yatakufanya umsahau. Anza kujiwekea desturi ya kutafuta amani ya moyo katika sehemu za kujiliwaza. Kama ulikuwa huna utaratibu wa kutoka kama kwenda bichi au muvi, anza sasa.

Ni bora kumlilia mtu ambaye anatambua thamani ya pendo lako kuliko kuteseka na mtu ambaye hatambui mchango wako. Haijalishi mlikuwa na ahadi gani katika penzi lenu, kama ameamua kukuacha, achana naye.

Tena usikurupuke wala usidanganyike harakaharaka kuanzisha uhusiano mpya. Utaumia kwa mara nyingine.

Huku ukiinjoi maisha ya kuwa peke yako na marafiki wa kawaida, muombe Mungu akupe mke au mume mwema ambaye atathamini penzi lako. Ataheshimu hisia zako. Atakuwa nawe kwenye raha na shida. Siku zote maishani chagua maisha ya furaha. Kataa maisha ya kuteseka kwa mapenzi.
Tukutane wiki ijayo kwa mada nyingine nzuri.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi