Oratilwe Hlongwana jina lake kamili maarufu Dj Arch Junior mwenye kipaji cha ajabu katika fani ya muziki.Anaheshima na kukubalika.Anauwezo wa kupiga muziki club za usiku na radio.Umri wake mdogo miaka mitatu ndio kivutio kikubwa anamashabiki maelfu pia wanamuziki wakubwa wa South Africa wanatambua uwepo na uwezo wake.
Mtaalam wa swaga zote za upigaji mziki anajua kucheza na tan table na akili za mashabiki.Inaweza ikawa bahati ya kuzaliwa nchi iliyo endelea ila kipaji kinambeba na kumweka alipo.kimombo wanasema kid got talent.


0 comments:
Post a Comment