- Sheria inaanza kutumika siku iliposainiwa so thread za zamani hazina matatizo ila thread mpya ambazo hazina FACTS wala EVIDENCE zitakuwa ni tatizo sana cha muhimu ni tujifunze kuandika kwa RESPONSIBILITY, juzi nimepitia ishu kama hii Owner wa Samaki Samaki Carlos alialikwa Ikulu akaonana na Rais ni muwekezaji kutoka nje amabye amewekeza sana hapa Tanzania ana anatoa ajira nzito sana kwa wananchi wengi sana hapa Dar,
- Baada ya picha zake kupigwa akiwa na Rais Ikulu, kuna mtu kwenye Social Media akachukua zile picha na kuziandikia habari chafu sana akimshambulia Carlos kwamba ni muuza madwa ya kulevya, MWanasheria wa Carlos alipomnasa mtu huyu akaanza kulia lia tu kuomba msamaha now jiulize watu kama Carlos bila SHERIA kama hii ingekuwaje? Niambie vipi washiriki wake wa kibiashara kama wamesoma ule upuuzi now wanamuonaje?
- I mean huenda kuna vipengere hii Sheria ina mapungufu lakini in the Big Picture hii sheria ni jawabu la kilio cha wanyonge wengi ambao wamekuwa wakitukanwa hasa hapa bila ya sababu, nimeipitia hii ishu sana ku deal na watu waliotukanwa hapa nimejionea kina mama wakilia machozi kwa kutukanwa hapa bila sababu za msingi, nimejionea watu wazima wakihangaika kuhusiana na threads walizoanzishiwa hapa zisizokuwa na ukweli, nitakupa mfano mwingine siku moja ilianzishwa thread kubwa hapa kwamba Malecela amemshambulia Lowassa habari ambayo haikuwa na tarehe wala location ya Malecela alimtukania wapi Lowassa, ile thread imekaa hapa kama wiki nzima ina page karibu 20 mpaka siku moja nikauliza tu eti haya maneno aliyasemea wapi na lini mara nikaona ile thread imetolewa kabisa,
- Now vitu kama hivi ambavyo tumevifanya wenyewe ndio vimepelekea Sheria kama hii, I mean haiwezekani watu wakishakuwa maarufu au Viongozi wa Taifa waanze kuishi kwa wasi wasi kwa sababu ya Social Media na Magazeti uchwara ambayo yaanaandika bila FACTS au EVIDENCE, mmeambiwa kwamba kama Sheria ina mapungufu andikeni pelekeni Wizara husika yakashugulikiwe which is a fair game badala yake mnali lia tu kwamba Sheria mbaya,
- Halafu kila mkiongea hamna hoja nzito so far, mimi siamini mambo mengi yalioandikwa kwenye Sheria mpya yatafanyika ila ninaamini kuna ya msingi sana ambayo yanajibu kwa uhakika tatizo la muda mrefu sana la Social Media in Tanzania ya matusi na kashfa zisizokuwa na FACTS wala EVIDENCE halafu ninashangaa ni wananchi wa Taifa gani Duniani ambao ni mpaka wafundishwe na Serikali yao kwamba kuandika bila ukweli au ushahidi ni makosa nilidhani wananchi wote wa Tanzania tulitakiwa kujua hilo bila hata hii sheria mpya, jamani tulikuwa tumepotoka tukubali sasa turudi kwenye mstari,
- JF kuna wakati tulipoanza tulikuwa tunaandika FACTS tupu bila uzushi wala majungu and then something I do not know happened pakaanza kuwa vurugu mechi, kuna wakati ilikuwa umeleta post bila FACTS inafutwa na wewe unaonywa au unafungiwa kwa muda, lakini leo that is not the case mtu anakurupuka anaandika anything hata bila FACTS au EVIDENCE halafu leo unakuta mtu yule yule analia lia unalia nini hivi unajua umeumiza wananchi wangapi na uongo wako hapa?
- Binafsi nimeshuhudia kesi moja ya Marehemu Komba, Msichana anayeitwa Angela anaishi Kiondoni Biafra alienda Karikaoo akaibiwa simu yake the next thing ni kuona picha zake kwenye Social Media na habari nzito kwamba anatembea na marehemu baada ya wataalamu hao wa Viwanda vya uongo kuziunganisha picha msichana na Marehemu zionekane kama ni kweli, ninakumbuka kumona yule msichana akilia machozi na mpaka kiuhama mji kwa karibu mwaka mzima kisa uzushi wa kwenye Social Media, so mnapolalamika sana kuhusu Sheria mkumbuke kuna wananchi wenye makovu mazito sana yaliyosababishwa na kinachorekebishwa sasa na Serikali,
- Poileni sana mlioathirika na hii Sheria ila pia muwakumbukumbe na walioathirika kwa muda mrefu sana na uongoz na majungu ya ajabu kwa kutokuwepo kwa hii sheria na wao ni wananchi wa Tanzania pia kama nyinyi ok!!
Le Mutuz Nation
source:- JF

0 comments:
Post a Comment