Posted by Williammalecela.com on Tuesday, May 05, 2015
Stori: Waandishi wetu
KONDAKTA wa daladala inayopiga kazi njia ya Makumbusho na Gongo la
Mboto, jijini Dar aliyetambulika kwa jina moja la Saidi (pichani),
ameingia matatani baada ya kudaiwa kuishi kinyumba na mwanafunzi wa
kidato cha tatu, tukio lililotokea Magomeni Kagera hivi karibuni,
kinyume na sheria za nchi.
Kondakta
wa daladala Saidi anayedaiwa kuishi kinyumba na mwanafunzi.Kwa mujibu
wa chanzo cha habari hizo, denti huyo mwenye umri wa miaka 17 anayesoma
Shule ya Sekondari Nguvu Mpya, iliyopo Chanika, Dar aliishi chumbani
kwa konda huyo baada ya bibi yake anayeishi naye maeneo ya Sinza, Dar
kusafiri kuelekea Zanzibar.
Ilidaiwa kuwa wawili hao wamekuwa wakiishi kama mke na mume tokea Machi, mwaka huu ambapo konda huyo akitoka humfungia ndani.
Denti
anayedaiwa kuwekwa kinyumba na konda.Ndani ya chumba cha konda huyo,
waandishi wetu wakiwa na polisi, walishuhudia sare za shule pamoja na
begi na madaftari na katika upekuzi kwenye madaftari hayo, ilionekana
mara ya mwisho aliandika Machi, mwaka huu.
Hata hivyo, kondakta huyo hakuwepo nyumbani wakati wa tukio hilo, lakini
polisi wameahidi kumsaka na kumkamata ili kumfikisha mbele ya sheria.
Akiwa
na mabegi yake kuelekea polisi.Mwanafunzi huyo aliliambia Uwazi kuwa
alikutana na konda huyo katika gari lake ambapo alikuwa akimpatia unafuu
wa usafiri bila kunyanyaswa kama inavyowatokea wanafunzi wengine kabla
ya kuanza uhusiano wa kimapenzi.
Alipoulizwa kuhusu wazazi wake, alidai mama yake alishafariki na
hakuwahi kumuona baba yake, akidai anaishi na bibi yake maeneo ya Sinza,
Dar ingawa hivi sasa amesafiri kwenda Zanzibar.
0 comments:
Post a Comment