,./.,

,,

... ...

';';';';

''=

==

adv
Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Sunday, May 24, 2015

Unapenda Selfie?
Vingi vimesikika, wapo waliokamatwa kwa sababu walipiga selfie maeneo ambayo hawaruhusiwi kufanya hivyo, hawa jamaa nao wamejikuta wakipoteza kibarua baada ya kukiuka maadili ya kazi yao kwakujipiga selfie.
Ni madaktari na manesi, walikuwa chumba cha operation Hospitali ya Shaanxi, China wakiwa wanaendelea na jukumu lao basi ikatokea wazo la kupiga selfie, wakati mgonjwa akiwa hana fahamu kalazwa akisubiri kufanyiwa upasuaji. Kitendo cha kushare
picha hizo kwenye mitandao ya kijamii kilipelekea madaktari na manesi kadhaa kfukuzwa kazi, huku wengine watatu wakikabiliana na adhabu ya kukatwa mshahara wa miezi mitatu kila mmoja.

Uongozi wa Hospitali hiyo umeomba radhi kwa kitendo hicho, huku ukisema kuwa wafanyakazi hao walichukua picha hiyo kama kumbukumbu ya siku yao ya mwisho kuwa kwenye chumba hicho kabla hakijafungwa kwa ajili ya kufanyiwa matengenezo.


0 comments:

Post a Comment

ufunguzi