,./.,

,,

... ...

';';';';

''=

==

adv
Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Monday, April 13, 2015




Mwigulu Nchemba NA Zitto Kabwe WAMEKANUSHA TAARIFA ZA UZUSHI.

TAARIFA KWA UMMA.

"Nimesoma taarifa zinazoenezwa kwenye mitandao ya kijamii zikionesha mawasiliano ya kugushi kati yangu na Ndugu Zitto Zuberi Kabwe. Taarifa hizo ambazo zinaonesha kuwa zimeandikwa kwa njia ya mtandao wa email, inataja jina langu na email ya shimbi85@gmail.com kama email yangu jambo ambalo ni uzushi na uongo.
 

Naomba kukanusha habari hizo na kusisitiza kuwa hiyo si email yangu na wala mawasiliano hayo si yangu kabisa.
Ukweli ni kwamba uzushi huo ni sehemu ndogo ya uzushi mwingi unaoenezwa na watu wasio na nia njema dhidi yangu kwa lengo la kunichafua kisiasa.
 

Katika kipindi hiki cha miezi ya kuelekea kwenye uchaguzi mkuu tutegemee kuona na kusoma uzushi mwingi na mkubwa kuliko huo utakaokuwa ukisambazwa kwa lengo au malengo sawa na haya."
 
Mwigulu Nchemba
Naibu katibu Mkuu CCM Bara na Naibu waziri wa Fedha.
13/04/2015

1 comment:

  1. kitendo cha Lema kuzozana na kiongozi wa Serikali kilaaniwe

    ReplyDelete

ufunguzi