Mwanzo wa yote nataraji kuwa wote mko salama na mnaendelea vyema na uchapaji kazi kama kawaida.
Rejea
kichwa cha habari hapo juu,tunaomba mtu peperushie hii habari ili
wahusika wajue kitu wanachokifanya sio sawa na wasijaribu kutuburuza
bila kutumia busara na kufuata sheria.
Ukitazama kwenye
attachment utaona tangazo la TBS ambalo wanatangaza kuanzia tarehe
16/03/2015.Kuna kampuni binafsi inayomilikiwa na watanzania hapa
Uk,ambao wanasemekana wameshinda zabuni ya kukagua magari yote
yanayotarajiwa kuja Tanzania kwa gharama ya $200 kwa kila gari,hii ni
uonevu na unyanyasaji kwa Watanzania wenzao,kwa sheria za UK kila gari
inahitaji kukaguliwa na kutambulika kama ina hali ya kuendelea kuwa
barabarani(MOT) ambayo kwa sasa iko digital,kupitia link za DVLA au
VOSA gonga hapa.Hii
MOT inafanywa na wataalamu walio bobea na wenye vifaa maalum,kwa magari
madogo vituo viko kila mji na kwa maroli na mabasi kuna vituo
maalumu,kwa magari madogo gharama yake ni £50 tu .
Tunasikitishwa
kwa kitendo cha TBS kutangaza mzabuni huyu bila kufuata ushauri wa
watanzania na wa kisheria ili zoezi zima liweze kukubalika na bila
kuwaumiza watanzania.Iweje leo tulipie $200 kwa kampuni binafsi wakati
kuna MOT yenye kiwango kuliko hii ya mtu binafsi na kwa pesa kubwa
zaidi?Na hii kampuni inauwezo gani wa kukagua maroli na mabasi yenye
kutaka kusafirishwa wakati ukaguzi wa hii unafanywa katika vituo
maalum?Hii kampuni itakuwa na vituo vingapi ili kuweza kukidhi matakwa
ya watanzania waishio UK.
Kwa kigezo kuwa kuna fake MOT,hiyo link juu ni sehemu ambayo kila mtu anaweza tizama uhalali wa MOT kwa kila gari iliyotoka UK.
Kifungu
kipi cha sheria kinatumika kuweka kiwango hiki?,kulikuwa na kesi
imefikia wapi hadi leo watujulishe kuwa kuna mzabuni na gharama hizi
kubwa.Hii ni aina ya uongozi usio jali maslahi ya watanzania na wasio
weza wapunguzia mzigo wenzao kisa matakwa yao binafsi ya kujitajirisha
tu.Mfano mzuri ni kuwa mtu yuko North katika miji kama Leeds au
Sheffield,ambako kuna vituo vya MOT lakini kwa utaratibu huu anapaswa
kuleta gari yake London,Tulibury port kwenye ofisi hizi binafsi kisha
atume gari yake.Wakati kuna vituo vya MOT kila mahali na kuna bandari
North sio lazima kuleta gari London.Huu si uhungwa hata kidogo.
Watanzania
wote walioko UK wanapinga utaratibu huu mpya wa kuhujumu watanzania na
kuomba serikali na shirika lake la viwangi kusitisha zoezi hili mara
moja na kutizama utaratibu mzuri wa kutumia MOT za serikali.
Kwa pamoja watanzania wa UK wameanza kuweka sahihi ya kuomba kusitishwa utaratibu huu gonga hapa kwenda kwenye petition.Tunaomba
kuwajulisha wahusika hali hii haitaweza kukubalika kwa sasa wala baadae
kwa kuwa huu ni mradi wa kunufahisisha watu wachache tu.Tunatanguliza
shukrani kwa wana habari wote wenye kusambaza habari hii na kuomba
wananchi wajiandikishe kupinga hali hii ya uonevu na unyanyasaji.
Ni sis wana
Diaspora UKTz
NB;
Link ya petition.
Ikiwa hapo juu haipatikani
http://www.change.org/p/![]() |
Friday, March 13, 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 comments:
Post a Comment