Na Lorietha Laurence- Maelezo
Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imewekeana saini na Serikali ya Japan kiasi cha shilingi bilioni 77,350,000 kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa barabara za juu katika makutano ya Tazara.
Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Fedha Dkt. Servacius Likwelile amesema kuwa mradi huo ni muhimu sana katika kukuza uchumi wa nchi na hivyo utasaidia kupunguza msongamano kwa wananchi.
“ Serikali ya Tanzania inathamini mchango wenu katika kusaidia kuboresha miundo mbinu ya barabara nawahakikishia kuwa fedha hizi zitatumika kama zilivyokusudiwa” alisema Dkt. Likwelile

Aliongeza kuwa kwa kupitia barabara hizo za juu bidhaa kutoka Bandari ya Dar es Salaam na Uwanja wa Ndege wa kimataifa zitasafirishwa kwa urahisi na haraka na hivyo kuchochea uwekezaji katika jiji hili la kibiashara.
Naye Kaimu Balozi wa Japan nchini Kazuyoshi Matsunaga alisema kuwa mkataba na mkandarasi kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo unategemewa kusainiwa Mei mwaka huu na kazi ya ujenzi kuanza rasmi .
“Mradi huu wa barabara ya juu wa Tazara utaanza kujengwa rasmi mara baada ya kuweka saini katika mkataba na mkandarasi atakayehusika na ujenzi na hivyo kusaidia katika kuepusha msongamano wa wasafiri na usafirishaji. “alisema Balozi,Matsunaga
Serikali ya Japan na Tanzania imekuwa ikishirikiana katika mambo mbalimbali ya kimaendeleo na kisiasa zaidi ya wa miaka 50 na hivyo kuimarisha mshikamano na umoja katika kukuza na kuinua uchumi wa jamii zote mbili.
0 comments:
Post a Comment