PROFESA Mwesiga Baregu, mmoja wa watu wanaoheshimika nchini amesema, aliyepata kuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, anaponzwa na kibuli cha kujiona hakuna zaidi ya yeye. Anandika Saed Kubenea … (endelea).
Amesema, Zitto ambaye alikuwa naibu katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (Chadema), Tanzania Bara na naibu kiongozi wa upinzani
bungeni, anafanya kazi asiyoifahamu na ambayo haina mavuno.
“Ninamfahamu
vizuri. Wakati tuhuma hizi za usaliti zilipoanza kuibuka, Kamati Kuu
ilinikabidhi jukumu la kumsaidia mama yake mzazi kumlea kijana huyu.”
Kauli ya Baregu ilitolewa siku moja baada ya Zitto kujiondoa bungeni na baadaye kujiunga na Chama cha ACT – Tanzania.
Prof. Baregu aliwahi kuwa “mlezi wa Zitto” ndani ya Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Alikabidhiwa jukumu hilo na Shida
Salum, mama mzazi wa Zitto (marehemu), baada ya mama huyo kuiomba Kamati
Kuu (CC) ya chama hicho “kusaidia kumlea.”
Prof. Baregu ambaye ni mjumbe wa kamati kuu ya Chadema anasema, “Zitto
hamnazo. Amekuwa anajiona yeye ni zaidi ya chama. Hashauriki.”
Anasema wakati ule alipopewa kazi ya kumlea Zitto “katikakati ya
migogoro, tulikuwa tunazungumza naye mara kwa mara. Ninamfahamu. Kazi
hii ya kumlea tulikabidhiwa mimi na mama yake mzazi, Bi. Shida Salum,”
anaeleza Baregu.
Mama mzazi wa Zitto, alifariki dunia Juni mwaka jana, baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Kauli
ya Prof. Baregu ilifuatia gazeti hili kutaka maoni yake juu ya
mustakabali wa kisiasa wa Zitto baada ya kuwahi kujiondoa ndani ya
Chadema.
Chanzo ni Mwanahalisi.online
>>video: The dramati
Wewe mzee baregu ni mnafki, utajivunjia heshima kujiingiza katika malumbano yasiyo na tija yeyote kwako. Zito ameondoka katika chama chako wala hajamtukana au kubeza mtu., iweje sasa wewe povu likutoke kinywani kumjadili kwani kaacha nini huko chadema, au kazungumza nini kuhusu wewe kama si ushambenga. Keep quiet !
ReplyDeleteNani kasema eti baregu ni mmoja wa watu wanaoheshimika? Anaheshimika na nani? Kauli anayotoa baregu kwa zito haimpi heshima ila inamshushia heshima, ni mpuuzi fulani tu.
ReplyDelete