,./.,

,,

... ...

';';';';

''=

==

adv
Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Saturday, March 14, 2015

Mhe. Sophia Simba ( Mb) Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto akizungumza (alhamisi) katika majadiliano ya jumla katikamkutano wa Kamisheni 59 kuhusu Hadhi ya Wanawake. Mhe. Waziri anaongoza ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwamo wajumbe kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.Tanzania ni kati ya nchi 13 zinazoiwakilisha Afrika katika Kamisheni hii inayoundwa na nchi 45.
Katika picha hii ya maktaba anaoneka Mhe. Asha-Rose Migiro ( Mb) wakati huo akiwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akiwa na baadhi ya askari wanawake kutoka JWTZ wanaoshiriki katika operesheni ya kulinda amani kupitia Umoja wa Mataifa huko Lebanon. Katika mchango wake, Mhe. Simba pamoja na mafanikio mengine ambayo Tanzania imeyapata katika miaka 20 tangu mkutano wa Beijing ni pamoja na askari wanawake kupata fursa za kushiriki katika operesheni za kulinza amani zinazoratibiwa na Umoja wa Mataifa.
Pamoja na kuzungumza katika majadiliano ya jumla, Mhe Waziri Sophia Simba pia alipata fursa ya kuhushiriki Mkutano wa Mawaziri kutoka Afrika uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Afrika karibu na UN. Mkutano huo ulikuwa wa kujadiliana na kupitisha maazimio mbalimbali kuhusu maudhui ya mwongo wa wanawake wa Afrika. Pichani Mhe. Waziri akiwa na Katibu Mkuu wake Bi. Anna Maembe wakifuatilia majadililano hayo
Sehemu ya ujumbe wa Mawaziri kutoka nchi za Afrika wakati wa mkutano wao uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Nchi za Afrika

Na Mwandishi Maalum, New  York

Ushiriki wa askari wanawake   katika Operesheni za Ulinzi wa Amani za  Umoja wa Mataifa,  ni baadhi ya  mafanikio ambayo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inajivunia miaka 20 baada ya Mkutano wa Kihistoria wa wanawake uliofanyika Beijing, China mwaka 1995
Waziri wa  Maendeleo ya Jamii, Jinsia na  Watoto, Mhe. Sophia Simba ( Mb) ameyasema hayo  leo ( alhamis) wakati alipokuwa akitoa tathmini na changamoto za utekelezaji wa  maazimio muhimu yaliyofikiwa katika mkutano huo wa  wanawake Beijing.
Mhe. Waziri Simba, anaongoza ujumbe wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania  katika Mkutano wa Hadhi ya Wanawake ( CSW) unaoendelea hapa  Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa,  katika Ujumbe huo  wa Tanzania unajumuisha na washiriki kutoka  Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akiwamo  Mhe. Zainab Omar Mohammed,  Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, vijana, wanawake na watoto, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi