1. Kila siku appointment zake yeye ni
gheto kwake au anang'ang'ania kuja
kwako, hakuna hata kwenda beach wala
hotelini.
2. Siku ukiwa unaenda kwake,
anakwambia njoo kwenye saa tisa au
kumi. Ujue amekadiria hiyo mida utakuwa
umeshapata lunch.
3. Ukiwa unaenda kwake hasemi
ukikaribia nishtue nitoke kukupokea, ujue
anaogopa akifika kabla yako itabidi alipie
bajaji.
4. Ukiwa unaondoka kwake anasema
sijisikii vizuri kwahiyo siwezi
kukusindikiza, ujue anaogopa unapopanda
bajaji itabidi akulipie.
5. Ukimwambia umefulia, anakwambia
"pole mpenzi ndiyo maisha hayo" ujue
hana cha kukupa.
6. Mkiwa mpo mahali inabidi kila mtu
aondoke peke yake ukasikia anasema
mimi nitapanda bajaji pale mbele kuna
sehemu napitia, ujue hana hela anaenda
kupanda daladala.
7. Kila mkienda kula restaurant jamaa
anasema "mimi nimetoka kula sio muda
njaa haiumi" haagizi hata maji ya kunywa
ujue jamaa hana kitu.
8. Kama upo mtandao tofauti na yeye
kila siku yeye anatuma tu sms, siku
akitaka kupiga simu anakwambia "weka
line ya tigo tuongee" ujue hana kitu huyo.
9. Ukiona anasisitiza kwamba hapendi
wanawake wanaopenda vitu vya gharama
kama simu n.k, ujue kaishiwa huyo akaoe
ma house girl.
10. Ukiona kila siku ukikaa nae anakupa
wosia kwamba mapenzi sio pesa, ujue
hana kitu huyo.
0 comments:
Post a Comment