Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, akifungua Mkutano wa 59 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hadhi ya Wanawake ( CSW), Mkutano huu wa wiki mbili ulioanza siku ya jumatatu, unafanyika ikiwa ni miaka 20 tangu kufanyika kwa mkutano wa kihistoria wa wanawake uliofanyika Beijing, China mwaka 1995. Mkutano huo uliokuwa chini ya Ukatibu Mkuu wa Dr. Gertrude Mongella, uliweka misingi mbalimbali iliyolenga katika kusimamia na kutetea haki mbalimbali za mwanamke zikiwamo za usawa wa kijinsia na uwezeshwaji.
Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi akiwa na sehemu ya Ujumbe wa Tanzania unaoshiriki Mkutano wa 59 wa Kamisheni kuhusu Hadhi ya Wanawake ulioanza jana jumatatu hapa Umoja wa Mataifa
Sehemu wa washiriki wa mkutano wa 59 wa Kamisheni kuhusu Hadhi ya Wanawake wakifuatili hotuba za ufunguzi zilizotolewa na viongozi mbalimbali akiwamo Katibu Mkuu Ban Ki Moon na Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Bw. Sam Kutessa
Na Mwandishi Maalum, New York
Mkutano wa 59 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hadhi ya Wanawake maarufu kama CSW umeanza rasmi siku ya jumatatu kwa hotuba za ufunguzi kutoka kwa viongozi mbalimbali akiwamo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon
Mkutano huu wa wiki mbili, unafanyika sambamba na maadhimisho ya miaka 20 tangu kufanyika mwaka 1995 huko Beijing , China, mkutano wa kihistoria uliowakutanisha wanawake kutoka maeneo mbalimbali duniani.
Dr. Gertrude Mongela, ndiye aliyekuwa Katibu Mkuu wa mkutano huo wa Beijing, uliotoka na tamko lililoweka misingi iliyolenga pamoja na mambo mengine, kutetea na kuimarisha hadhi ya mwanamke, usawa wa kijisia na uwezeshwaji wa wanawake.
Katika siku ya kwanza ya mkutano huo, wajumbe pamoja na kusikiliza hotuba za ufunguzi pia walipitisha kwa kauli moja, Tamko la Kisiasa linalosisitiza dhamira ya ya matokeo ya mkutano wa kihistoria wa wanawake uliofanyika Beijing mwaka 1995.
0 comments:
Post a Comment