,./.,

,,

... ...

';';';';

''=

==

adv
Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Monday, March 9, 2015


 Mkurugenzi Mr Mrisho Masud Inshallah katika meza kuu
 Mkurugenzi wa Ok Electrical Ltd Mrisho Masud Inshallah na kikundi cha line ya Kineng"ene na Nangaru

  Mkurugenzi wa Ok Electrical Ltd Mrisho Masud Inshallah na kikundi cha line ya Ngongo Village kinahusisha vijiji 11 na katika vijiji hivyo vijiji 7 tayari vimepata umeme na kubaki vijiji 4 kukamilisha utalatibu mzima katika mradi.
 Mkurugenzi wa Ok Electrical Ltd Mrisho Masud Inshallah na kikundi cha line ya Mchinga 1via Mkwajuni kinacho husisha vijiji 5 kama Kilangala,Mvumbila,Kitomanga,Mkwajuni na Mipingo wakiwa katika picha ya pamoja katika hafla.


 Madereva wa Kampuni ya Ok Electrical Ltd wakiwa katika picha ya pamoja 

 Mkurugenzi wa Ok Electrical Ltd Mrisho Masud Inshallah na kikundi cha line Mchinga 2 mpaka Mpingo via Mkwajuni katika line hii kwa asalimia 70 uwekaji wa waya pamoja na nguzo wamekamilisha kwa sehemu kubwa na wamekuwa na matarajio ya kumaliza mapema mnamo mwezi wa 4 katika kuenda sambana na makamilisho ya mradi huu unao tarajia kuisha mwezi wa 6 mwaka huu.
 Hassan Mrisho ni Store Kipper Akiwa katika hafla 
 Ni ndugu Johakimu Peter Malia ni Project Menager wa Ok Electrical Ltd ila kwa siku hii ya tukio alikuwa akisimama kuongoza shughuri za hafla kuanzi utangulizi wa mwanzo mpaka mwisho wa shughuri nzima.
 Wafanyakazi wa Ok Electrical wakiwa katika mazingira ya nje ya office wakijadiliana na kubadilishana mawazo mbali mbali juu ya utendaji kazi na changamoto zake zinazowakali.
 Mkurugenzi wa Ok Electrical Ltd Mrisho Masud Inshallah akiendelea kufunguka na kutoa maelezo jinsi gani inahitajika kufanya kukabilia na matatizo wanayopata mafundi wanapokuwa site katika utendaji wao kuzingatia umuhimu wa kazi na kujari thamani ya wafanyakazi wake mkurugenzi alitoa msisitizo kwa wafanyakazi juu ya ufanyaji kazi kwa bidii na kuongeza kujitahidi kadri ya uwezowake kusimamia na kuyafanya yale ambayo wafanyakazi wake walikuwa wameomba ayafanyie kazi.

 Mkaguzi Ndugu Mohamed Mcharo akitoa maneno machache kwa nafasi yake baada ya kupewa nafasi ya kuzungumza na wafanyakazi wa Ok Electrical Ltd.
Katika mradi huu wa Ok Electrical ulianza mapema mwaka 2014 na unatarajiwa kukamilika mnamo mwaka huu 2015  katikati mwezi wa sita.

Kwenye mradi huu kwa ulipo fikia Alisema Mkurugenzi Mrisho Masud kuwa  sasa umefikia asilimia 70% kukamilija kabisa na kubadilisha lindi kuwa katika muonekano wa tofauti katika upande wa nishati  kutokana na wanavijiji kukaa miaka mingi bila kupata umeme na hatimaye Ok Electrical Ltd inawafanikishia kwa kuwaletea umeme majumbani kwao.

Ingawa kila panapo kuwa na chembe ya mafanikio lazima changamoto ziwepo lakini kwa Ok Electrical zimekuwa changamoto za kuwafanya wazidi kusonga mbele katika utendaji kazi mwanzo mwisho mpaka wafikew kwenye malengo waliyo pangwa.

Kuna line nyingi tofauti tofauti katika kukamilisha mradi huu ambao umekuwa mkubwa na wenye manufaa kwa wana lindi kwa asilimia 100%.

Line Route 1 inaanzia kijiji cha Ngongo Village mpaka Milola kwenye vijiji hivyo kuna vijiji vingine vinavyo nufaika na mradi huu kama 
1:Ngapa Nkupima
2:Ngapa Mbuyuni
3:Narunyu
4:Tandangongoro
5:Rutamba
6:Nambawala
7:Chilala FDC
8:Kinyope
9:Legeza Mwendo
10:Milola
Line Route 2 inaanzia kijiji cha Mchinga mpaka Mpingo via Mkwajuni kuna vijiji vingine vinavyo nufaika na mradi huu 
1:Kilangala
2:Mvumbila
3:Kitomanga
4:Mkwajuni
5:Mpingo

Line Route 3  inaanza katika kijiji cha Mchinga 2  mpaka Mvuleni hadi Kijiweni kukiwa na vijiji vinavyo nufaika na mradi huu ikiwemo vijiji kama
1:Mnangote
2:Kilolambwani
3:Maroho
4:Mvuleni A
5:Mvuleni B
6:Kijiweni

Kwenye Line hii wamefanikiwa akutandaza nguzo za umeme kwenye maeneo yote pamoja na uwekaji waya ukiwa umebakiza asilimia chache sana kukamilika katika mradi huu.

Line Route 4 inaongozwa na Living Mushi nakuanzia kijiji cha Mtange Village na Nangaru kukiambatana na vijiji kama 
1:Kining"ene
2:Chikonji
3:Moka
4:Matimba
5:Kikomolela
6:Nangaru
katika vijiji hivi wamekamilisha vijiji vi 3 na vimebaki vijiji 3 kukamilisha kwa upande huu.

Line Route 1 kwa upande  wa Kilwa  Kingi (4way) na  Kipa timu Village  muongozaji akiwa Flavian Mulawa kukiambatana na vijiji kama 
1:Mingumbi
2:Wamayuni
3:Chumo A
4:Chumo B
5:Nasaya
6:Darajani
7:Kipatamu

Line  Route 2 Kwa upande wa vijiji vya Nanguvukuvu na Miguvuwe vikiwa na vijiji 
1:Migeregere
2:Kipitimbi
3:Njinjo
4:Selou
5:Miguvume

Line Route 3 Manzese mpaka Matandu ikiwa inavijiji vichache 
1:Mtandango
2:Miteja
3:Sinza
Kwenye line hii hakuna tatizo lolote mradi umekamilika kwa asilimia 100% na wanakijiji wa vijiji hivi wanapata umeme safi kabisa.
Ok Electrical imekuwa kampuni inayo ajiri vijana na kuwapatia ajira nakujiopoa kwenye majanga tofauti hususani hili la madawa ya kulevya kwa vijana wengi wa lindi wamekuwa wakipata ajira kwa wingi kadri kampuni inapokkuwa inahitaji wafanyakazi wapya wakuopngeza nguvu katika kampuni.

Mategemeo ya mradi huu iifikapo mwezi wa 6 itakuwa mwisho wa mradi huu na itakuwa ok Electrical imekamilisha kwa asilimia 100% kuwapatia wanavijiji wa mkoa wa lindi umeme kwa kila upande ni hatua ambayo italeta mabadiliko na kufikia malengo ya serikali kufikia mwaka 2016 vijiji vyote nchini viwe vimepata nishati ya umeme bila kipingamizi chochote.

Hivyo ndivyo ilivyokuwa katika mkoa wa lindi kwenye hafla ya kampuni ya OK ELECTRICAL LTD kuonyesha wamefikia wapi na malengo yao niyapi katika kufikia kipindi cha mwisho cha kumalizia mradi kwa kujua mengi juu ya kampuni hii ya umeme ya Ok Electrical Ltd usikae mbali na blogu yetu tutakujulisha hapo hapo ulipo upatikanaji wa kazi pamoja na miradi mipya inayoanzishwa na kampuni hii.


Categories:

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi