Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Valentino Mlowola (kushoto) akionyesha baadhi ya nyara walizokutwa nazo waganga hao.
Baadhi ya tunguli na nyara za serikali walizokutwa nazo waganga hao wasiokuwa na leseni.
Waganga hao pia walinaswa wakiwa na bendera ya taifa ambayo inadaiwa kutumiwa na wanasiasa pindi waendapo kwa waganga hao.
JUMLA
ya waganga wa kienyeji 55 wasiokuwa na leseni wamekamatwa mkoani Mwanza
katika oparesheni iliyofanyika kuanzia Machi 6, mwaka huu.
Akiongea
na wanahabari leo jijini Mwanza, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza,
Valentino Mlowola amethibitisha kukamatwa kwa waganga hao 55 ambapo kati
ya hao 18 ni wanawake na 55 wakiwa wanaume.
Oparesheni
hiyo inayoongozwa na Kamanda Mlowola bado inaendelea ili kuhakikisha
kuwa waganga wote wanaopiga ramli chonganishi wanakamatwa na kuhakikisha
kuwa usalama wa maalbino unakuwepo na wanaishi kwa amani kama wananchi
wengine.
Aidha
Kamanda Mlowola ameongeza kuwa waganga hao wamekamatwa na nyara
mbalimbali za serikali zikiwemo ngozi za wanyama kama simba, kenge,
ngozi za mijusi, ngozi za vinyonga vilivyokauka na vitu vinavyosadikika
kuwa ni nywele za albino pamoja na meno ya albino lakini amesema kuhusu
meno na nywele ataoa majibu sahihi baada ya Mkemia Mkuu wa Serikali
kufanya vipimo juu ya vitu hivyo
0 comments:
Post a Comment