Katibu wa Uenezi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Longido Ndugu Onesmo Steven Maarufu kwa jina la SIMON amekihama Chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo katika Mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana, katika viwanja vya Eworendeki, Namanga.

Mwenezi huyo wa Chadema amefikia hatua hiyo baada ya kuona kuwa CHADEMA ni chama cha kibabaishaji ambacho hakina mwelekeo na wanatumia siasa za kilaghai kudanganya wananchi na kuifarakanisha jamii.

Kinana amempokea Mwenezi huyo kutoka CHADEMA na kusema kuwa Chama Cha Mapinduzi kinawakaribisha wale wote ambao wamegundua ulaghai wa Upinzani na kwamba CCM haina ubaguzi kwani kila mwanachama ana haki sawa na mwingine, hakuna kuoneana wala upendeleo.