,./.,

,,

... ...

';';';';

''=

==

adv
Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Saturday, March 14, 2015

Basi la Simiyu Express linalofanya safari zake Dar - Simiyu kila siku limepata ajali kwa kugonga mkokoteni unaosukumwa na ng'ombe na kuua mtu mmoja na ng'ombe wote leo saa sita mchana
mkoani Simiyu katika kijiji cha Salunda barabara kuu iendayo Shinyanga.
Hakuna abiria aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa ila kiongozi wa mkokoteni.dereva alifariki dunia na ng'ombe wake wawili walifariki pia.

Basi aina ya Scania lenye namba za asajili T396 AMP
Kampuni ya Simiyu Express mali ya Adinan Khan Mkazi wa Dar es salaam linalofanya safari zake Mkoani Simiyu-Dar es salaam, likiwa kwenye kichaka baada ya kupata ajali muda mfupi baada ya kutoka stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.

Inaelezwa kuwa baada ya kuacha njia likiwa katika mwendo kasi lilikutana na mkokota toroli la ngo'mbe akiwa katikati ya barabra maeneo ya Salunda kata ya Bariadi Mjini .
Kufuatia hali hiyo basi hilo lilimgonga mkokota toroli aitwaye Bahati Suti (25) Mkazi wa Musoma wilayani Itilima Mkoani Simiyu ambaye alifariki dunia papo hapo , huku ngo'mbe 2 na wakipoteza uhai papo hapo.
Kamanda wa polisi Mkoani Simiyu Charles Mkumbo amesema basi hilo lilikuwa likiendeshwa na Ramadhan Hassan (30) mkazi wa Magomeni Kagera Jijini Dar es salaam, na kwamba kufuatia ajali hiyo gari hilo liliharibika kioo cha mbele pamoja na bampa na dereva wa basi anashikiliwa na jeshi la polisi.Abiria wote 34 katika basi hilo ni wazima.
Baadhi ya wasamaria wema wakikokota mkokoteni uliosababisha ajali hiyo na kupoteza uhai wa dereva wake pamoja na Ngo'mbe 2.
Baadhi ya mashuhuda wakiangalia basi hilo
Mashuhuda.
Ngo'mbe akiwa amekufa
Baada ya basi kutolewa kichakani, muonekano wake lilivyopata ajali




0 comments:

Post a Comment

ufunguzi