
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Askofu Gehazi Malasusa (wa pili kutoka kushoto) na viongozi wengine wa Serikali wakiwa kwenye dhifa ya kitaifa ya chakula cha usiku aliyoandaliwa Rais wa Ujerumani Joachim Schadt na Rais Jakaya Kikwete jana usiku jijini Dar es salaam.

Rais wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete na mgeni wake Rais wa Shirikisho la Ujerumani Mh. Joachim Gauck wakielekea sehemu ya nyuma ya ukumbi kutazama Brass bendi ya Jeshi la Polisi iliyokuwa ikitoa burudani wakati wa dhifa ya kitaifa ya chakula cha usiku aliyomuandalia mgeni wake jana usiku Ikulu jijini Dar es salaam.

Rais wa Shirikisho la Ujerumani Mh. Joachim Gauck akitoa ujumbe wake kwa wageni mbalimbali waliohudhuria dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Rais Jakaya Kikwete Ikulu.

Rais wa Ujerumani Mh. Joachim Gauck na Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania wakitazama vikundi mbalimbali vya ngoma za asili vilivyokuwa vikitumbuiza wakati wa dhifa ya kitaifa Ikulu jijini Dar es salaam.

Rais wa Shirikisho la Ujerumani Mh. Joachim Gauck (wa pili kutoka kulia) akiteta jambo na Rais mstaafu wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi jana usiku wakati wa dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Rais Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam. Kushoto ni mke wa Rais wa Ujerumani Bi. Daniella Schadt na mama Sitti Mwinyi Mwinyi.
Rais wa Shirikisho la Ujerumani Mh. Joachim Gauck (wa pili kutoka kulia) akiteta jambo na Rais mstaafu wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi jana usiku wakati wa dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Rais Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam. Kushoto ni mke wa Rais wa Ujerumani Bi. Daniella Schadt na mama Sitti Mwinyi Mwinyi.
Mkuu wa wilaya ya Temeke Sophia Mjema (kushoto) akiongea na baadhi ya wageni waalikwa akiwemo Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Diana Melrose (aliyesimama) wakati wa dhifa ya kitaifa ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na Rais Jakaya Kikwete kwa Rais wa Ujerumani Mh. Joachim Gauck , Ikulu jana usiku.
Rais wa Shirikisho la Ujerumani Mh. Joachim Gauck na Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania wakitazama Brass Bendi ya Jeshi la Polisi iliyokuwa ikitumbuiza wakati wa dhifa hiyo Ikulu jijini Dar es salaam.
0 comments:
Post a Comment