Posted by Williammalecela.com on Tuesday, February 17, 2015
 |
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Janeth Mbene yupo ziarani
Dubai. Katika ziara hiyo, Mhe. Mbene ameutembelea Ubalozi Mdogo wa
Tanzania uliopo Dubai na kufanya mazungumzo na Mhe. Omar Mjenga, Balozi
Mdogo wa Tanzania. Aidha, Mhe. Mbene amepata maelezo ya kina kuhusu
shughuli za Ubalozi Mdogo na Kituo cha Biashara.
Mkurugenzi
wa Kituo cha Biashara Ndugu Ruhumbika, amemueleza Mhe. Mbene ni kwa
jinsi gani Ubalozi Mdogo kwa kushirikiana na Kituo hicho wameweza
kuvutia wawekezaji wengi kwenda Tanzania.
Kwa
upande wake, Mhe. Mjenga amemuomba Mhe. Mbene kuwa Serikali iangalie
uwezekano wa kujenga ofisi zake za Ubalozi Mdogo ambazo zitakuwa na
nafasi kubwa kwa ajili ya maonyesho ya bidhaa za Tanzania kwa muda wa
mwaka mzima. Nchi nyingi zilizo na Ubalozi Mdogo na Kituo cha Biashara
hapa Dubai, wameweza kuvutia uwekezaji na uuzaji wa bidhaa za biashara
zinazotoka kwenye nchi zao kwa utaratibu huu.
Pichani, ni Mhe. Mjenga akimkaribisha Mhe. Janeth Mbene ofisini kwake kwa mazungumzo.
|
0 comments:
Post a Comment