Staa wa muziki wa kizazi kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
IMEKULA kwake! Wasanii wa sinema na Bongo Fleva wamemchana vibaya staa wa muziki wa kizazi kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kwamba si mtokaji kwenye misiba ya wenzake.Wakizungumza na Amani kwenye maziko ya baba mzazi wa Mbongo Fleva, Abdul Sykes ‘Dully Sykes’, Ebby Sykes, Jumatatu iliyopita, wasanii hao walioomba majina yao yalindwe walisema kumbukumbu za vichwani mwao zinaonesha kuwa, Diamond amekuwa akichagua misiba ya kujitokeza hasa ile ambayo itampa ‘kavareji’ kwenye vyombo vya habari.
“Mimi nakumbuka wakati wa kifo cha Kanumba (Steven), Diamond alitokea kwa sababu ulikuwa msiba mkubwa sana na kweli alipata kavareji ya kutosha kwenye media.
“Halafu akaonekana tena kwenye msiba wa baba yake Wema Sepetu, nadhani kwa vile alikuwa mtu wake Wema wakati huo asingeacha kwenda. Lakini baada ya hapo sikumbuki,” alisema msanii mmoja.
Msanii mwingine aliongeza: “Halafu Diamond na Dully ni washikaji, sasa jamaa tunasikia yuko Zenji tu hapo anakula bata na Zari (Zarina Hassan) lakini ameshindwa kuja Dar kumzika baba mzazi wa mshikaji wake.”
0 comments:
Post a Comment