Ile kesi ya maadili,
iliyofunguliwa na
Sektarieti ya Maadili ya
viongozi wa umma,
imeanza kunguruma
katika ukumbi wa
mikutano hapa Karimjee
jijini Dar es Salaam.
Mtuhumiwa ni Prof. Anna
Kajumulo Tibaijuka.
Mbunge huyo wa Muleba
Kusini (CCM), ametinga
ndani ya chumba cha
"mahakama" tayari kujibu
tuhuma zinazomkabili juu
ya ukiuwaji wa sheria ya
maadili ya viongozi wa
umma.
Prof. Tibaijuka
anatuhumiwa kujipatia
kiasi cha Sh. 1.6 bilioni
kutoka kwa James
Rugemalira.
Anatuhumiwa
"kumshawishi"
Rugemalira kumpa fedha
hizo.
Yeye amekana madai
hayo. Kesi imeanza.
0 comments:
Post a Comment