Posted by Williammalecela.com on Thursday, February 26, 2015
 |
Hakimu
wa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, leo ametoa
hukumu ya kifungo cha miaka miwili jela au kulipa faini kwa rapper,
Chidi Benz.
Chidi alipandishwa kizimbani mahakamani hapo kusomewa mashtaka matatu ya
kukutwa na madawa ya kulevya mwaka jana. Alikuwa nje kwa dhamana ya
shilingi milioni 1 pamoja na wadhamini wawili wasiokuwa na hatia.
Faini anayotakiwa kulipa ni shilingi laki tisa. Chidi alikutwa na madawa
ya kulevya aina ya heroin yenye thamani ya shilingi 38,638, na bangi
yenye thamani ya shilingi 1,720 pamoja na na vifaa ya kuvutia dawa hizo
ambavyo ni kijiko na kigae.
Tukio hilo lilitokea October 25 mwaka jana katika uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akiwa anaelekea jijini
Mbeya kwenye show.
Chanzo: bongo5 |
0 comments:
Post a Comment