,./.,

,,

... ...

';';';';

''=

==

adv
Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Tuesday, February 17, 2015


Mwanamuziki maarufu nchini wa muziki wa kizazi kipya Ommy Dimpoz leo mchana kwa saa za Marekani amejikuta katika wakati mgumu sana na maofisa wa uhamiaji wa nchi hiyo baada ya kumkatalia kuingia Marekani
alikokuwa amekwenda kwa ajili ya show mbili za muziki wake moja New York City na nyingine Los Angeles. Habari za ndani sana toka huko USA zinasema Dimpoz alikuwa amekwenda bila kibali kinachoruhusu kwenda kufanya kazi nchini humo kwa wasanii wote wanaotoka nje ya nchi hiyo kama sheria ya Taifa hilo inavyosema ikiwa na nia ya kuwabana Wasanii walipie kodi kazi zao wanapofanya matamasha yao kule, kwa hiyo kuikwepa hiyo wakamchukulia Viza ambayo inaonyesha anaenda kule kama mtembezi tu, sasa cha ajabu ni kwamba maofisa hao wa uhamiaji wa Marekani tayari walikuwa na Fliers zinazo onyesha Dimpoz atapiga muziki New York City, Brooklyn na Los Angeles ka wa hiyo Dimpoz akaulizwa amekwenda US kufanya nini? Akajibu "Nimekuja kutembea", akaonyeshwa fliers zake na kuulizwa huyu kwenye flier sio wewe? Akajibu kweli ni yeye akaulizwa mbona hakusema ukweli? Safari ikashiwa hapo hapo na kuambiwa asubiri the next flight ya kurudi kitendo ambacho kina maana moja kubwa kwamba hataruhusiwa kuingia nchi hiyo kwa miaka 10 ijayo. Utata wa Uhamiaji wa Marekani kuwa na fliers zinazo onyesha matamasha ya Dimpoz ina maana moja tu kwamba kuna promota aliyewashitua Uhamiaji wa huko mapema sasa swali ni kwa nini afanye hivyo? Bado ni kitendawili kikubwa ambacho tunategemea kukitegua soon!! - Blogu ya Wananchi

1 comment:

  1. Hahaha hahaha aaaaaaahhhhh umeona eehhh lahaulaaaa

    ReplyDelete

ufunguzi