“Namfahamu
kocha Phiri (Patrick), ni kocha mzuri, nilifurahi kufanya naye kazi
kipindi nikiwa timu ya Taifa na yeye akiwa Simba, nina imani kuwa ujio
wake utaongeza changamoto kwenye ligi na ubingwa utakuwa mgumu zaidi
msimu ujao,” Maximo
Imechapishwa Agosti 16, 2014, saa 7:06 mchana
BAADA
ya kutua nchini, kocha wa Simba Patrick Phiri alishtuka kusikia
Mbrazili Marcio Maximo yupo Yanga na sasa jamaa amemjibu Phiri akisema:
“Ndio nipo Yanga nimejaa tele.” Akaendelea na mambo yake.
Maximo
amesema ushindani mkubwa wa namba ulioko kwenye kikosi cha klabu hiyo
umewafanya baadhi ya wachezaji wanaougua malaria kutaka kuendelea na
mazoezi badala ya kupumzika.
“Namfahamu
kocha Phiri (Patrick), ni kocha mzuri, nilifurahi kufanya naye kazi
kipindi nikiwa timu ya Taifa na yeye akiwa Simba, nina imani kuwa ujio
wake utaongeza changamoto kwenye ligi na ubingwa utakuwa mgumu zaidi
msimu ujao,” alisema Maximo
Akizungumzia
wachezaji wake, Maximo alisema: “Ushindani wa namba kwenye kikosi
changu umekuwa mkubwa, nafarijika kuona kila mchezaji anataka kucheza,
hiyo inanipa imani kuwa nitakuwa na kikosi bora msimu ujao.”
Chanzo: Mwanaspoti
0 comments:
Post a Comment