Nyundo hiyo: Nyota wa Swansea City, Gylfi Sigurosson alifunga bao la ushindi jana .
ALAN Shearer amemuonya kocha wa Manchester United, Louis van Gaal kuwa anahitaji kusajili wachezaji watatu wa kiwango cha dunia kama anataka kukaa nafasi nne za juu.
Mashetani wekundu wana mipango kabambe ya kurudi ligi ya mabingwa barani Ulaya mwakani, lakini jana kikosi cha Mholanzi kinachosumbuliwa na majeruhi kilichapwa mabao 2-1 na Swensea City katika mechi ya ufunguzi wa ligi kuu soka nchini Englnd ndani ya dimba la Old Trafford.
Mchambuzi wa mecni, Shearer alisema jana kuwa kipigo cha Manchester United kinaweza kuwa mwanzo wa kuvurunda tena.
Alisema: 'Kiwango kilikuwa kibovu na matokeo mabaya yalipatikana, hii inaweza kuwa mwanzo mbaya tena, lakini nawaambia matajiri wa Manchester United kuwa wanahitaji kusajili angalau wachezaji watatu wa kiwango cha dunia".
"Wanahitaji kutumia fedha nyingi kupata wachezaji wa kiwango cha juu kama wanataka kukabiliana na changamoto ya kuingia timu nne za juu"
Mwanzo mgumu: Louis van Gaal anafahamu kuwa ana kazi ngumu katika klabu ya Manchester United.
0 comments:
Post a Comment