,./.,

,,

... ...

';';';';

''=

==

adv
Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Tuesday, August 27, 2013

HALMASHAURI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo imemamliza kikao chake cha siku tatu chini ya Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete ikiwa imeridhia mapendekezo kadhaa ya Kamati Kuu ya CCM, ikiwemo kumfuta uongozi Mbunge wa jimbo la Mjini Magharibi, Zanzibar, Mansor Yusuf Himid.

Kikao hicho pia kimeridhia, uteuzi wa Makatibu wateule wapya wa Jumuia za CCM, za Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Jumuia ya Wazazi na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT).

Katika uteuzi huo mapendekezo hayo yaliyofanywa na Kamati Kuu ya CCM, na kuridhiwa na NEC, kwa upande wa Umoja wa Vijana wa CCM ameteuliwa aliyekuwa Kaimu Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro, Sixtus Mapunda na kwa upande wa Jumuia ya Wazazi ni Mjumbe wa NEC kutoka Pemba, Seif Shabani Mohamed, huku kwa upande wa UWT akiachwa Katibu Mkuu wa sasa, Amina Makilagi.

Mapunda atachukua nafasi iliyokuwa imneshikiwa na Martine Shigela ambaye ameongoza UVCCM kwa miaka mitano sasa, na Seif Shabani Mohammed kutoka Pemba akichukua nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Hamis Suleiman Dadi ambaye pia amekuwa katika wadhifa kwa miaka mitano sasa.

Pia, NEC imeridhia mapendekezo ya Kamati Kuu kwa ajili ya kuziba nafasi Makatibu wa CCM wa mikoa mitatu ya Morogoro, Kaskazini Pemba na Geita ambayo kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa imekuwa wazi kwa muda mrefu sasa kutrokana na sababu mbalimbali ikiwemo kifo.

Kufuatia mapendekezo hayo ya Kamati Kuu, ambayo yameridhiwa na NEC, walioteuliwa na mikoa yao ikiwa kwenye mabano ni Msaidizi Kitengo cha Uchaguzi, CCM Ofdisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Romuli Rojas John (Morogoro), aliyekuwa Katibu Katibu wa wilaya ya Mkinga, Kassim Mabrouk Mbarak (Kaskazini Pemba) na aliyekuwa Katibu wa CCM Igunga, Mary Maziku (Geita).

Kuhusu sakata la madiwani wa Bukoba mjini, CCM imesema suala hilo, linaendelea kushughulikiwa ambapo baada ya kikao hicho cha NEC, Kamati kuu iliendelea kukutana na viongozi wa wilaya ya Bukoba, Mwenyekiti wa CCM na Katibu wa wilaya hiyo.

Mapema kabla ya kikao cha NEC, Kamati Kuu ilikutana na Mbunge wa Bukoba mjini Khamis Kagasheki na Meya wa Manispaa ya Bukoba mjini na kuwahoji, wakati jana Kamati Kuu ilikutana na Mwenyekiti na Katibu wa CCM mkoa wa Kagera.

Majina ya Makatibu wa Wilaya walioteuliwa,

1. Ndugu Ashura Amanzi
2. Ndugu Rukia Saidi Mkindu
3. Ndugu Elias J. Mpanda
4. Ndugu Jonathan M. Mabihya
5. Ndugu Mulla Othman Zuberi
6. Ndugu Jumanne Kapinga
7. Ndugu Ali Haji Makame
8. Ndugu Jacob G. Makune
9. Ndugu Juma A. Mpeli
10. Ndugu Hawa Nanganjau
11. Ndugu Abdulrahman Shake
12. Ndugu Subira Mohamed Ameir
13. Ndugu Abdallah Shaban Kazwika
14. Ndugu Juma Bakari Nachembe
15. Ndugu Josephat Ndulango
16. Ndugu Rajab Uhonde
17. Ndugu Abeid Maila
18. Ndugu Mohamed Lawa
19. Ndugu Mariam Sangito Kaaya
20. Ndugu Bakar Lwasa Mfaume
21. Ndugu Julius Peter
22. Ndugu Jumanne Kitundu Mginga
23. Ndugu Mathias Nyombi
24. Ndugu Mohamed Hassan Moyo

Kidumu Chama Cha Mapinduzi.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi