Waziri
Mkuu Mstaafu wa Zamani Dk.Salim Ahmed Salim akifungua Baraza la
Katiba la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika
mchakato wa mabadiliko ya Katiba lililofanyika leo kwenye ukumbi wa
mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dares Salaam.
Picha Eleuteri Mangi –maelezo.
BARAZA
la Katiba la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
limependekeza kuwa Watanzania waliopo nje ya nchi wasifutiwe uraia wa Tanzania.
Kauli
hiyo ilitolewa na Waziri wa Mambo Nje ya Ushirikiano wa Kimataifa,
Bernard Membe wakati alipokuwa akichangia suala la uraia katika mchakato
wa mabadiliko ya Katiba kupitia baraza hilo kwenye ukumbi wa mikutano
wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dares Salaam.
“Raia
wa Tanzania aliyeko nje ya nchi na kuomba uraia wa nchi hiyo kwa sababu
yoyote ile iwe ya elimu , afya au ajira asifutiwe uraia wa Tanzania,”
alisema Waziri Membe.
Waziri
Membe aliongeza kuwa Watanzania waliopo nje ya nchi ambao ni waaminifu
hawawezi kupata ajira rasmi ‘white collar job’ hivyo kuishia kufanya
kazi zisizo rasmi.
Alifanunua kwa Watanzania walioamua ‘kujilipua’ yaani kuukana uraia wamepata
kazi nzuri lakini hawasaidii taifa lao la asili.
Kauli hiyo ya Waziri Membe iliungwa mkono wa baadhi ya mabalozi waliotumikia Tanzania katika nchi mbalimbali wakati mjadala huku wakitaka suala liwekewe utaratibu ili kuokoa nguvu kazi ya taifa na wataalamu mbalimbali walioko nje ya nchi.
kazi nzuri lakini hawasaidii taifa lao la asili.
Kauli hiyo ya Waziri Membe iliungwa mkono wa baadhi ya mabalozi waliotumikia Tanzania katika nchi mbalimbali wakati mjadala huku wakitaka suala liwekewe utaratibu ili kuokoa nguvu kazi ya taifa na wataalamu mbalimbali walioko nje ya nchi.
Miongoni
mwa mabalozi waliounga mkono ni Balozi Martin Lumbanga ambaye alisema
“Suala la uraia wa nchi mbili ninaliunga mkono kwa kuwa lina faida
nyingi kuliko hasara,”alisema.
Balozi
Paul Rupia alisema wakati umefika kwa Watanzania kuwa na uraia wa nchi
mbili, hivyo suala hilo lisiogopwe bali liwekewe utaratibu unaofaa.
“Ni vema tuliwekee utaratibu ili tuendelee kuwa na watu wetu bila kuwapoteza,”alisema Balozi Rupia.
Kwa mujibu wa Waziri Membe alisema hivi sasa Watanzania waliopo nje ya nchi ni milioni tatu kati ya Watanzania zaidi milioni 44.
Baraza
hilo lilihudhuriwa na mabalozi hao, makatibu wakuu kiongozi wastaafu,
na watumishi mbalimbali wa wizara hiyo ambapo aliazimia suala hilo
liingizwe kwenye mchakato wa rasimu ya Katiba.
0 comments:
Post a Comment