Basi la Yanga
Alisema kuwa baada ya kumfanyia uchunguzi Msuva,
ikaonekana kuwa hakuumia sana kiasi cha kushindwa kucheza mechi ya kesho
dhidi ya Coastal Union iliyopangwa kufanyika kwenye Uwanja wa
Mkwakwani.
Mwandishi Wetu
MSAFARA wa Mabingwa wa Soka wa Afrika Mashariki na Kati, Yanga umevamiwa na wahuni wanaosadikiwa kuwa ni mashabiki wa timu ya Coastal Union na mchezaji wake chipukizi, Simon Msuva amejeruhiwa.
Tukio hilo limetokea jana saa 5.00 asubuhi wakati kundi kubwa la wahuni waliojikusanya maeneo ya Michungwani na Kabuku kupiga mawe basi la Yanga walilopewa hivi karibuni na Kampuni ya Bia ya Tanzania (TBL).
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa klabu hiyo, Seif ìMagariî Ahmed alisema kuwa wakiwa wametulia katika gari hilo, ghafla walisikia mawe yakipiga basi lao ambayo yalivunja kioo cha basi hilo na kuzua tafrani.
Alisema kuwa kutokana na hali hiyo, wachezaji walipatwa na hofu na kuanza kuhangaika, huku jiwe lingine likivunja kioo na kumdondokea Msuva aliyekuwa karibu na dirisha na kumpiga kichwani.
ìIlikuwa hali ya kutisha sana kwani hata Kabuku nako tulipatwa na mkasa huo na kuamua kukimbilia polisi na kutoa taarifa, hali haikuwa nzuri na bahati yetu gari lilikuwa katika mwendo na kuwafanya warusha mawe kushindwa kufanya uharibifu zaidi na hata kujeruhi wachezaji wetu,î alisema Seif.
Alisema kuwa baada ya kumfanyia uchunguzi Msuva, ikaonekana kuwa hakuumia sana kiasi cha kushindwa kucheza mechi ya kesho dhidi ya Coastal Union iliyopangwa kufanyika kwenye Uwanja wa Mkwakwani.
Polisi wa Usalama wa Barabarani alithibitisha kuwapo kwa tukio hilo kwa njia ya simu.
Trafiki huyo alisema kuwa aliona gari la klabu hiyo kituoni na kupata taarifa za kupigwa mawe likiwa njiani katika maeneo hayo mawili.
ìBasi la Yanga lilifika hapa saa 5.00 hivi na baada ya kutoa taarifa, wakaruhusiwa kuendelea na safari, hakukuwa na majeruhi wa kutisha sana zaidi ya huyo mchezaji aliyegongwa na kioo na kuvunjika kwa kioo,alisema.
Seif alisema kuwa uongozi wa Yanga umesikitishwa na tukio hilo ambalo limewatishia amani kwani ni mara ya kwanza kukumbwa na mkasa huo hasa wakiwa njiani kuelekea Tanga.
ìHii ni mara ya kwanza, sasa sijui hao waliofanya hivyo walikuwa wanataka nini. Hii ni Ligi Kuu ya Tanzania Bara, tunapaswa tucheze mpira kwa amani ndani na nje, sasa mambo haya ya kupigwa mawe yanatokana na nini? Hali hii haitupendezi,î alisema Seif.
Yanga hivi sasa inaongoza Ligi Kuu ikiwa na pointi 26 na ikishinda mechi ya kesho itakuwa imejikita kileleni kwa kufikisha pointi 29.

0 comments:
Post a Comment