MBUNGE wa Viti Maalumu wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mwanamrisho Taratibu Abama jana
asubuhi aliugua na kuanguka ghafla katika viwanja vya Bunge na
kukimbizwa hospitali....
Tukio hilo lilitokea wakati akienda
kuhudhuria semina ya wabunge kuhusu Rasimu ya Sera ya Gesi Asilia kabla
ya kukosa nguvu na kudondoka na kisha kusaidiwa na wenzake
kumkimbiza kwenye zahanati ya Bunge.
Baada ya kupatiwa huduma ya kwanza
bungeni, gari la wagonjwa lilimkimbiza Hospitali ya Mkoa wa Dodoma
(General) ambako amelazwa.
Kwa mujibu wa waliomshuhudia, mbunge
huyo alianza kwa kuishiwa nguvu hali ambayo waliokuwa karibu
walimsaidia kumpeleka kwenye zahanati ambako alitundikiwa dripu kabla
ya kupelekwa hospitalini.
Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Dodoma, Zainabu Chaula alikiri kumpokea mbunge huyo.

0 comments:
Post a Comment