WAZIRI AMCHARUKIA JACK WA CHUZ!!
BAADA
ya hivi karibuni msanii wa filamu, Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’
kunaswa akipelekwa kuuzwa kwa mwanaume, Naibu Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo, Amos Makalla anadaiwa kuicharukia skendo hiyo
ambapo juzikati alimvaa Rais wa Shirikisho la Filamu (TAFF), Simon
Mwakifwamba na kumuuliza juu ya tukio hilo la aibu.
Chanzo
cha habari kutoka ndani ya shirikisho hilo kililitonya Ijumaa kuwa,
Mhe. Makalla alimvaa Mwakifwamba kwenye mkutano na wasanii uliofanyika
ndani ya Hoteli ya Kibadamu, Ubungo jijini Dar.
“Mhe.
Makalla ndiye aliyekuwa mgeni rasmi, akiwa pale alimuuliza Mwakifwamba
kuhusu hatua walizochukua kwa Jack Chuzi baada ya kuandikwa habari kuwa
alinaswa akienda kuuzwa.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla.
“Mwakifwamba
alijitetea kuwa, wanalishugulikia na Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji
Tanzania, Michael Sangu ‘Mike’ akasisitiza kuwa, wako katika mchakato wa
kulitolea uamuzi tukio hilo lililofanywa na Jack ,” kilidai chanzo
hicho.
Baada
ya kuzinyaka habari hizi paparazi wetu alimtafuta Mwakifwamba lakini
hakuweza kupatikana mara moja ila Mike alipoulizwa juu taarifa za Mhe.
Makalla kucharukia ishu ya Jack alisema:
Rais wa Shirikisho la Filamu (TAFF), Simon Mwakifwamba.
“Ni
kweli waziri aliuliza kuhusu hatua tulizozichukua kuhusu suala la Jack
kujiuza ambapo nilimjibu kuwa tuko kwenye mchakato wa kulitolea uamuzi
na kwa sasa tumeunda kamati maalum, ikimaliza uchunguzi wake ndiyo
tutatoa jibu kuwa tumemchukulia hatua gani.”
0 comments:
Post a Comment