Wafuasi wa Ponda waachiwa kwa dhamana
Katibu wa Kamati ya kutetea haki za Waislamu,Sheikh Ponda Issa
Ponda(katikati) na wenzake 49 wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu aliposomewa mashtaka ya uchochezi na kuvamia kiwanja kilichouzwa
na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania(Bakwata) jijini Dar es salaam.
Kwa ufupi
“Dhamana iko wazi kwa washtakiwa wa pili hadi wa 50,
kwa kuwa makosa yao yanadhaminika isipokuwa mshtakiwa wa kwanza tu, kwa
sababu DPP alileta certificate (hati) ya kuzuia asipewe dhamana,”
Mashtaka manne yanawahusu washtakiwa wote 50
isipokuwwa shtaka moja la uchochezi, ambalo linamhusu Sheikh Ponda pekee
anadaiwa kuwashawishi wafuasi wake kutenda makosa ya uhalifu.
Wakati kesi hiy ilipotajwa mahakamani hapo Novemba
Mosi, mahakama ilikubali kuwapa dhamana washtakiwa wote isipokuwa
Sheikh Ponda ambaye mahakama ilisema haina mamlaka ya kisheria kwa kuwa
DPP aliwasilisha hati ya kuzuia dhamana yake.
Siku hiyo Mwendesha Mashtaka, Wakili wa Serikali Mwandamizi (SSA), Tumaini Kweka alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika.
Siku hiyo Mwendesha Mashtaka, Wakili wa Serikali Mwandamizi (SSA), Tumaini Kweka alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika.
Hivyo, Kwaka aliomba mahakama ipange tarehe ya
usikilizaji wa awali (PH), washtakiwa hao watasomewa maelezo ya awali ya
kesi inayowakabili na kutakiwa kubainisha mambo wanayokubaliana na
wasiyokubaliana nayo.
Hata hivyo, Wakili wa washtakiwa hao, Juma Nassoro
alikumbusha mahakama kuhusu dhamana ya washtakiwa hao, akidai kuwa
wakati walipopandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza, maombi yao ya
dhamana hayakushughulikiwa kwa kuwa hakimu aliyepangwa kusikiliza kesi
hiyo hakuwapo.
Hakimu Nongwa alikubaliana na maombi hayo ya
dhamana na kusema dhamana iko wazi kwa washtakiwa wote, isipokuwa Sheikh
Ponda ambaye dhamana yake imefungwa na DPP.
0 comments:
Post a Comment