Mo Blog: Shibuda umekuwa mwanasiasa kwa siku nyingi nini rai yako kwa viongozi wenzio wa kiasiasa.?
Shibuda: Napenda kutoa rai kwa vyama na viongozi wa
kisiasa ambavyo viko karibu 21 hapa Tanzania, la kwanza kila chama
kijifanyie tathmini, kinawajibika vipi kutekeleza mipango ya kuendeleza
amani na utulivu katika hii nchi.
Vinatekeleza mipango gani? Na kila chama kifanye tathmini kijiulize
mambo gani ambayo ni makosa kwa ustawi na maendeleo ya nchi yetu
inaoongozwa na kulindwa na tabia, mila na desturi za Mtanzania.
Vyama vya siasa viwe na wito unaoitwa ‘kwa maslahi ya umma’ na viongozi pia watekeleze wito unaoitwa kwa maslahi ya umma.
Mo Blog: Kwani una shaka na baadhi ya vyama?
Shibuda: Vyama ambavyo vina mdudu shetani anayeitwa
ibilisi wa kujenga tafrani, migongano, misuguano au vyama vinavyoitwa
‘chama kampuni’ kwa maslahi binafsi, havistahiki kuwa sehemu moja wapo
ya mbegu ya kuzalisha amani.
Hivyo watanzania tutafakari, tusemezane, tutazame viwango vya kila
chama, katika vyama 21 kwamba je? Tija ya kila chama ni kwa kujenga
ustawi na maendeleokwa jamii? Ili mwaka kesho tusherehekee tena siku ya
amani duniani. Kusoma zaidi mahojiano yote ingia
www.mohammeddewji.com/blog
0 comments:
Post a Comment