Waranti huo unahusishwa na madai ya rushwa, lakini umetolewa wiki moja
baada ya serikali kufanikiwa kuzima mgomo wa wachimba migodi uliyokuwa
unaenea, na ambao Malema alikuwa akiutumia kumshambulia rais Jacob Zuma.
Hatua hiyoimekuja baada ya miezi kadhaa ya fununu kuwa Malema alikuwa
anachunguzwa kuhusiana na madai ya kupokea rushwa ili kuwasaidia
wahusika kupata zabuni za serikali.
Chanzo dewjiblog.com/
0 comments:
Post a Comment