MZEE SABODO KUCHANGIA UPINZANI SI TATIZO.
"Kuna watu wengi wanauliza nini maoni yangu juu ya uamuzi wa Mzee Sabodo kusaidia vyama vya upinzani na hasa Chadema.
Kimsingi sioni tatizo kwa Mzee Sabodo kuamua kusaidia vyama vya upinzani na wakati huohuo akabaki kuwa kada mwaminifu wa CCM.
Ikumbukwe ni serikali ya CCM ndio iliyobadili sheria kuruhusu
uanzishwaji wa mfumo wa vyama vingi! Hata baada ya kuviruhusu vyama
vingi bado ikatengeneza utaratibu wa ruzuku kwa vyama vya siasa! Yote
haya yamefanywa na serikali ya CCM.
Sasa kama serikali ya CCM
imefanya, cha ajabu hapa kwa mwanachama wake kufanya ni nini? Hivi
kwanini tunataka kuwafikisha watanzania mahali wasisaidiane kisa siasa!
Wapo wanaohoji kwanini Mzee Sabodo ametoa visima kwa Chadema?!! Sasa
najiuliza visima vitakapoanza kufanya kazi watumiaji wataulizwa itikadi
zao au kila mwananchi anauhuru wa kutumia?! Tatizo hapa ni nini?!
Narudia sioni tatizo kwa Mzee Sabodo kusaidia vyama vya upinzani ili mradi pesa hizo ni zake!!"
0 comments:
Post a Comment