Mama Caxx ni Model anaetikisa huko Marekani kutokana na uzuri wa rangi yake na hata umbo lake lilivyo.
Alizaliwa mwaka 1989 huko Brooklyn na baada ya hapo alikulia huko Haiti ambapo akiwa na umri wa miaka 14 aligundulika kuwa ana Kansa ya mifupa jambo ambalo lilimfanya akate tamaa.
Hata hivyo madaktari walisema ana wiki tatu za kuishi baada ya hapo anageweza kupoteza maisha yake kutokana na ugonjwa huo kusambaa kwa kasi katika kiungo chake.
Baada ya hapo Madaktari walijitahidi sana kumpatia dawa jambo ambalo walifanikiwa kufanikisha maisha yake na baada ya hapo ilibidi wamkate mguu wake mmoja.
Jambo la kukatwa mguu aliendelea kulizoea hadi alipofikia umri mkubwa kidogo akaingia katika maswala ya urembo na fasheni.
Mrembo huyo amekuwa akijiamini sana licha ya kuwa na mguu mmoja hajawahi kujiona tofauti kutokana na hali yake na watu wengi wamekuwa wakimfurahia sana na kupenda kazi zake za umodo.
Hivi karibuni katika mtandao wake wa Instagram alionekana akifanyiwa makeup na Mwanamuziki wa Marekani Rihana ambapo alikuwa akijiandaa na sherehe ya mambo ya urembo.
Kwa sasa Moda huyo anaishi huko New York Nchini Marekani ambapo ndipo anapofanya kazi zake za umodo na ameweza kufundisha watu wengi kuingia katika umodo na amekuwa akizunguka nchi nyingi Duniani zikiwemo za Afrika.

0 comments:
Post a Comment