Meneja wa kundi la Muziki la Sauti Sol Marek Fuchs na mkewe ambaye ni mwanamitindo nchini Nairobi wamepata Mtoto wa kiume na wamempa jina la Kenzo akiwa ni mtoto wao wa kwanza.
Marek ambaye amemuoa mwanamitindo Annabel Onyango amefurahia kupata mtoto wao ambapo wameonesha furaha na kuposti picha ya mtoto wao mtandaoni.
Marek na Annabel wanaishi Nairobi, walifunga ndoa mwaka 2015 nchini humo ambapo hadi sasa wanaendelea kuishi Nairobi mwanaume akiwa Meneja wa Saut Sol na Mke wake akiwa anaendelea na kazi zake za mitindo.
Meneja huyo wa Saut Sol ni raia Czech ambapo alikuja Nairobi tangu mwaka 2008, Mama yake akiwa Balozi nchini Nairobi.
Kundi la muziki la Saut Sol limempongeza Meneja wao na mkewe kwa kumapata mtoto wao wa kwanza ambapo wamekuwa wazazi wapya.

0 comments:
Post a Comment