
TAARIFA ZA HIVI PUNDE TOKEA DODOMA BUNGENI
Akiongea wakati akifungua Bunge asubuhi hii, Spika wa Bunge Job
Ndugai amesema haya;
"Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Tundu Lissu alifyatuliwa risasi kati ya 28-32.
Risasi 1 ilimpata mkononi, 2 tumboni na 2 mguuni. Spika amesema familia ya Lissu ndiyo iliyochagua ndugu yao kwenda kutibiwa Nairobi nchini Kenya lakini Bunge lilikuwa limejiandaa kumpeleka Muhimbili.
Serikali inaamini hospitali ya Muhimbili ni hospitali bora kabsa katika nchi za Africa Mashariki ndio maana iliona haja ya kumpeleka huko, lakini familia ikachagua kumpeleka Nairobi kwa ajili ya usalama wake.
Maneno mengine mnayo yasikia kwa wanasiasa sio ya kweli. Ni unafiki wao kila kitu kwao ni kiki ya kisiasa hata kwenye misiba wao wanafanya hivyo. Tumuombee apone kijana wetu #TunduLissu akiwa mzima wa afya ndipo turudi kwenye siasa zetu majitaka."
0 comments:
Post a Comment