Mkuu wa Jeshi la Polisi Saimon Sirro amewataka wale wote waliotajwa kwenye ripoti ya Tanzanite na Almasi waweze kujisalimisha wenyewe kwani wanajijua.
Amezungumza na waandishi wa habari leo ambapo amesema wao wameshafungua jalada hivyo wafike wenyewe kwa mahojiano na baada ya hapo sheria itachukua mkondo wake.
"Tumepokea taarifa kutoka kwa Rais hivyo tumeifanyia kazi na waliotajwa wanajijua wenyewe na wapo baadhi ya waliotajwa wameanza kupiga simu kuuliza wanatakiwa kuripoti wapi" amesema .
Kwa upande wa tukio la Mbunge wa Singida Tundu Lisu amesema wako nalo makini na wametuma wapelelezi Dodoma wakasaidie tukio la kuwasaka wahusika na wana uhakika watawapa waliofanya hivyo.
Aidha kuhusu tukio la utekaji wa watoto Jijini Arusha amesema msako bado unaendelea na Watanzania wawe na amani kwani mtuhumiwa mmoja ameshakamatwa na hata kama ameua kutokana na kutaka kutoroka lakini wengine watakamatwa tu.
Hata hivyo amesema kwa wakazi wa Kibiti na Rufiji hali ni shwali hivyo watanzania wanaweza kwenda kuendelea na kazi zao kama kawaida bila hofu wala wasiwasi.

0 comments:
Post a Comment