Utafiti
huo wa pamoja uliofanywa na wasomi kutoka Swansea, Australia na
Marekani ulifuatilia mbwa mwitu walio kwenye hatari ya kuangamia nchini
Botswana
Waligundua kuwa mbwa walitumia chafya kuamua wakati wanaelekea kuwinda
baada ya kufanya mikutano inayofahamika kuwa mikutano wa kijamii.
Awali ilikuwa ikifikiriwa kuwa mbwa hao ambayo ni familia ya wanyama
walio kwenye hatari zaidi ya kuangamia duniani, walikuwa wakipiga chafya
ya kawaida.
Lakini wakati watafiti walirekodi mikutano 68 ya mwa
mwitu waligundua kuwa wakati walipiga chafya zaidi walikuwa wakiondoka
na kuanza wa kuwinda.
Dr King anasema kuwa chafya hiyo ni lazima ifike kiwango fulani kabla ya wao kuamua kufanya kitu.
Pia uutafiti huo uligundua baadhi ya chafya huwa na uzito kuliko zingine.
0 comments:
Post a Comment