Posted by Williammalecela.com on Friday, September 08, 2017
Kesi ya Malinzi yapigwa kalenda tena
Kesi inayomkabili aliyekuwa Rais wa (TFF), Jamal Malinzi na wenzake wawili imeahirishwa baada ya hakimu anayesikiliza shauri hilo kuwa na dharura hapo jana.
Wakili wa Serikali, Faraj Ngokah ameieleza Mahakama ya Hakimu Kisutu
leo Alhamis, kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na Hakimu
anayesikiliza shauri hilo, Wilbard Mashauri ana udhuru.
"Washtakiwa wapo Mahakamani, lakini Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri
ana dharura, hivyo tunaomba tarehe nyingine kwa ajili kutajwa" alidai
wakili Ngokah.
Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa aliahirisha kesi hiyo September 21 mwaka huu itakapotajwa. Mbali na Malinzi, washitakiwa wengine ni Katibu wa TFF, Mwesigwa Selestine na Mhasibu wa shirikisho hilo, Nsiande Mwanga. Washtakiwa kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka 28, ikiwemo ya utakatishaji fedha. |
|
0 comments:
Post a Comment