Alikiba ambaye yupo midomoni mwa watu kutokana na wimbo wake 'Seduce me' kupokewa vizuri na watu na kuweza kuweka rekodi ndani ya masaa 38 kufikisha watazamaji milioni moja, Kiba amezidi kuwapoteza washindani wake kwa wimbo huo kuendelea kufanya poa.
Video ya Alikiba ambayo jana ilionekana kushuka kwa nafasi moja na kuwa namba mbili kwa video ambazo zilikuwa zinafanya vizuri Tanzania jambo ambalo liliwafanya baadhi ya mashabiki wa msanii huyo kuongeza kampeni katika mitandao ya jamii ili kurudi katika nafasi ya kwanza na kuhakikisha kuwa video hiyo inafikisha watazamaji milioni tatu ndani ya siku sita.
Mashabiki wa Alikiba waliweza kutimiza ahadi yao kwa kuifanya video hiyo kufikisha watazamaji milioni tatu ndani ya siku sita toka wimbo huo utoke jambo ambalo halijawahi kutokea katika historia ya muziki wa Alikiba.
Alikiba alikiri wazi kuwa alibadili gia angani na kuachia wimbo huu ambao haukuwa kwenye mpango wa kutoka na kusema wao walikuwa wamependekeza wimbo mwingine kutoka lakini baadaye wakasema waje na wimbo huu kwanza 'Seduce me' kabla ya kuanza kuachia ngoma zingine ambazo kwa mujibu wa mtayarishaji Man Water kuwa hizo ndiyo ngoma za moto zaidi.
0 comments:
Post a Comment