Mwanamuziki Saida Karoli, amesema kibao cha ‘Urugambo’ amekitoa kama kifungua kinywa, badala yake watanzania watarajie kupata nyimbo kali mfululizo.
Saida anasema nyimbo zinazofuata ni zile alizoimba akiwashirikisha Belle 9 na Diamond Platinumz.
“Urugambo nimetoa kama zawadi kwa Watanzania, niliona nijitambulishe kama chai ya asubuhi, lakini watarajie mambo makubwa kwani hivi karibuni mimi na Belle 9 tutatoa kazi ambayo itawatoa jasho mashabiki wa muziki,” alisema Saida.
0 comments:
Post a Comment