,./.,

,,

... ...

';';';';

''=

==

adv
Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Friday, June 30, 2017

Staa wa Bongo, Elizabeth Kimemeta Michael ‘Lulu’ akifanya yake na mchekeshaji kutoka nchini Kenya, Eric Moni stejini.
 Busu ‘makinikia’ alilomwagiwa na ‘mtoto mtamu’ kutoka Magufuli-landElizabeth Kimemeta Michael ‘Lulu’ limempa mawenge ya mwendokasi mchekeshaji kutoka nchini KenyaEric Mondi ambapo hakusita kuweka wazi hisia zake juu ya muigizaji huyo mwenye mvuto bomba.



Twitter Ads info and privacy
Akiwa jukwaani akitema madini yake ya vichekesho ndani ya Ukumbi wa King Solomoni jijini Dar siku ya Eid, Omondi alimtaja Lulu kama miongoni mwa wasanii wa kike Bongo wanaomvutia zaidi na bila kusita alimuita jukwaani kwa lengo la kupata japo wasaaa wa kupata busu lake, ombi ambalo Lulu alilitii na kilichofuata kinajieleza kwenye aya zinazofuata hapa chini.
Mara baada ya Lulu kupanda jukwaani, moja kwa moja alimfuata Eric na kumkumbatia kwa kumzungushia mikono kiuononi na kisha kumiminia mabusu mfululizo, hali iliyomchachawisha Eric na kupoteza ‘netiweki’ kwa muada, hali iliyoongeza shangwe miongoni mwa wahudhuriaji wengi.

“Mtoto safi sana nyie acheni tu, ni miongoni mwa wasanii kutoka hapa TZ wananivutiaga sana, tazama mwenyewe anavyojiseti aiseeee,” alisikika Omondi akimsifia Lulu  wakati muigizaji huyo akishuka jukwaani na kurejea kwenye sehemu yake ya kukaa.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi