,./.,

,,

... ...

';';';';

''=

==

adv
Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Sunday, May 7, 2017

Msanii wa filamu Shamsa Ford amefunguka na kumtetea Flora aliyewahi kuwa mke wa Emmanuel Mbasha ambaye wiki iliyopita aliolewa tena na kijana Daudi Kusekwa 

Shamsa Ford ameibuka na kuanza kumtetea Flora kutokana na maamuzi yake hayo ya kuolewa kwa mara ya pili na kusema yeye ndiye anajua kwanini ameamua kufanya hivyo na kumtaka kutosikiliza maneno ya watu.
"kwanza kabisaa ningependa kukupongeza kwa kuolewa dada yangu hakika mlipendeza sana. Dada yangu nina uhakika umekutana na mitihani mingi sana kwenye maisha yako na ukaweza kupambana nayo. Basi hata haya wanayoongea binadamu ona kama wanaimba mziki tu..Binadamu siku zote ni waongeaji hata uwafanyie nini hawawezi kuacha kuongea. Wewe ndiyo unayejua umuhimu na upendo wa mumeo basi inatosha. Hakuna binadamu anayepasa kumuhukumu binadamu mwenzie zaidi ya Mwenyezi Mungu pekee yake. Fanya unachoona ni sahihi kwako wewe na Mungu wako tu" alisema Shamsa Ford 
Shamsa aliendelea kusisitiza 
"Hizi kelele za binadamu zisikunyime raha wala amani dada yangu awe kijana, awe mzee, awe mdogo, awe masikini, awe tajiri, awe mbaya, awe mzuri yote haijalishi kwa sababu ni wa kwako na wala hujamuomba mtu akusaidie kukaa na mumeo...Inshaallah Mwenyezi Mungu aibariki ndoa yenu iwe ya furaha na amani" alisema Shamsa Ford 

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi