
Asubuhi ya leo May 6, 2017 imeripotiwa ajali mbaya iliyotokea Mlima Rohotia, Karatu mkoani Arusha ikuhusisha basi la wanafunzi ambao walikuwa wanakwenda kufanya mtihani wa ujirani mwema.
Taarifa za awali zinasema kuwa dereva wa basi la wanafunzi wa Shule ya LackVicent alishindwa kuliongoza vizuri basi hilo wakati akikata kona kwenye mteremko hivyo likaingia kwenye korongo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amethibitisha kutokea ajali hiyo akisema taarifa zaidi kuhusu ajali hiyo zitatolewa baadaye.


0 comments:
Post a Comment