Posted by Williammalecela.com on Tuesday, May 23, 2017
 |
Balozi wa Uingereza nchini Tanzania *Bi. SARAH COOKE,* amemtembelea Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe PAUL MAKONDA* na kufanya nae mazungumzo
yenye lengo la kuongeza na kuimarisha Ushirikiano uliopo baina ya jiji
la Dar es salaam na London, nchini Uingereza.
Katika mazungumzo
yao, *Mhe MAKONDA* na *Bi. COOKE* wamekubaliana kuongeza kasi ya
Ushirikiano baina ya majiji makubwa mawili *Dar es salaam* Tanzania na
*London* nchini Uingereza, makubaliano
ambayo yatasaidia kupatikana kwa vifaa vya kisasa vya kuzuia na
kupambana na majanga kama vile moto na mafuriko, ambapo *Mhe MAKONDA*
ameomba kupatiwa magari ya kisasa ya shughuli za kuzima moto na uokoaji.
*Mhe MAKONDA* pia ameomba kusaidiwa vifaa maalum vya *UTAMBUZ*I wa
mifumo ya teknolojia ya kamera za kisasa zitakazofungwa *barabarani* kwa
ajili ya kusaidia *USALAMA* wa magari, raia na mali zao mifumo ambayo
inafanya kazi katika jiji la London nchini Uingereza, hatua
itakayokwenda sambamba na ujengewaji *UWEZO* kwa maofisa wa *polisi* wa
Mkoa wa
Dar es salaam katika matumizi ya mifumo hii.
Katika
kukabiliana na changamoto ya *MIGOGORO ya ARDHI* mkoani Dar es salaam,
*Mhe MAKONDA* ameomba kusaidiwa kuwajengea uwezo *maafisa ARDHI* na
*Mipango miji* wa Mkoa wa Dar es salaam katika matumizi ya kisasa ya
upimaji na upangaji ardhi, mafunzo ambayo yatakwenda sambamba na
upatikanaji wa vifaa vya kisasa vya kupima ardhi, jambo litakalosaidia
*kuondoa KERO* ya upatikanaji wa *HATI* pamoja na *vibali vya UJENZI*
Mkoa wa Dar es salaam.
Katika mazungumzo hayo, *Mhe MAKONDA* na
*Bi. COOKE* wamejadili suala la uanzishwaji wa *JIJI la FIKRA* (brain
storming center ) kwa ajili ya kuwakutanisha vijana wabunifu kama ilivyo
kwa *Tech City Uingereza.*
Katika kuhitimisha mazungumzo yao,
*Mhe MAKONDA* na *Bi. COOKE* kwa pamoja wamekubaliana kuzikutanisha timu
za wataalamu kutoka London na Dar es salaam za kukabiliana na Majanga
haraka iwezekanovyo.
*Bi. COOKE,* kwa upande wake
*amefurahishwa* na jinsi Mkuu wa Mkoa anavyopambana na *vita ya dawa za
kulevya* ambayo imeathiri nguvu kazi kubwa sana katika jiji la Dar es
salaam na kumuhakikishia kuwa *Serikali ya Uingereza inaunga mkono
jitihada zote* zinazofanywa katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Mkoa
wa Dar es salaam.
*Imetolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam.* *23/05/2017.*
|
 |
|
 |
|
0 comments:
Post a Comment