
Hamisa Mobeto.
VIDEO queen matata Bongo, Hamisa mobeto amesema kwa sasa yupo bize na malezi ya mtoto hivyo taarifa za kwamba amerudiana na mzazi mwenziye ambaye ni bosi wa redio moja Bongo, hazina ukweli.
Hamisa Mobeto.
Hamisa alifunguka hayo baada ya kuulizwa na mwanahabari wetu juu ya taarifa zilizozagaa kwamba amerudiana na mzazi mwenziye huyo ambaye pia alihamishia majeshi kwa muigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Hamisa na Mwanaye.
“Naomba waniache kuniingiza kwenye mapenzi ya watu wengine, mimi huyo ni mzazi mwenzangu na itabaki kuwa hivyo, mambo mengine hayanihusu kabisa, niko bize kulea mtoto wangu, siwezi kurudi nyuma,” alisema.
Majizo na Lulu.



0 comments:
Post a Comment